Sunday, October 19, 2014

UZINDUZI WA MASHINDANO YA KUPIGA KASIA KWA UTHAMINI WA BIA YA BALIMI LAGER KANDA YA ZIWA YAFUNGULIWA LEO RASMI KIGOMA



UZINDUZI WA MASHINDANO YA KUPIGA KASIA KWA UTHAMINI WA BIA YA BALIMI LAGER KANDA YA ZIWA YAFUNGULIWA LEO RASMI KIGOMA
 Timu ya Nyika stars wakimalizia kupiga kasia kwenye Ziwa Tanganyika ambao ni mabingwa wa Mkoa na watauwakilisha Mkoa kwenye mashindano ya kanda tarehe 6 Novemba jijini Mwanza
 Washiriki wanawake wakipiga kasia katika mashindano ya kupiga kasia kwa kutimia mitumbwi ndani ya ziwa Tanganyika
 Washindani wakijiandaa na mchuano
 Washindi wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Ramadhani Maneno
Kiongozi wa washindi wa kwanza kwa upande wa wanawake kutoka kikundi cha Katonga Beach akionyesha kitita chake kwa mashabiki
Kiongozi wa kikundi cha wanaume cha Nyika Stars ambao ndo mabingwa wa Mkoa akionyesha kitita cha shilingi laki 9
Na Editha Karlo wa Globu ya Jamii, Kigoma
KAMPUNI ya bia Tanzania(TBL)kupitia bia yake ya Balimi Extra Lager imefanya uzinduzi wa mashindano ya mitumbwi ya  kupiga kasia kwa kanda ya ziwa leo Kigoma katika fukwe za eneo la ya Bangwe.

Akizindua mashindano hayo Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Ramadhani maneno ametoa shukrani kwa uongozi wa bia ya balimi Lager kwa kuupa Mkoa wa Kigoma heshima ya kuwa wenyeji wa uzinduzi wa mashindano hayo kikanda.

Maneno alisema kuwa mchezo siyo mpira pekee hata kupiga kasia pia ni mchezo pia kinachotakiwa ni wachezaji wote kuzingatia nidhamu na kufuata masharti na maelekezo pia aliwataka wadhamini kuongeza zawadi ili iwe kivutio kwa washiriki wengi kujitokeza mwakani.

''Nina waomba ndugu zangu mlioshinda katika vikundi vyenu fedha hizi tulizowapa isiwe ndiyo chanzo cha kwenda kulumbana bali mzitumie kwa uwekezaji na faida itakayopatikana katika uwekezaji huo ndo mgawane''alisema Mkuu wa Wilaya

Alisema kupitia mashindano hayo ya mitumbwi yanayofanyika kila mwaka Mkoani hapa ni njia mojawapo ya kuwaweka watu pamoja kushirikiana na kuboresha maslahi yao pamoja biashara zao.

Mashindano hayo yalishirikisha jinsia zote wanawake na wanaume,kikundi cha wanaume kiitwacho nyika Star kilifanikiwa kunyakua ubingwa wa kwanza na kuondoka na kitita cha shilingi laki tisa(900000)na upande wa wanawake kikundi kilichoongoza ni Katonga Beach nacho kiliondoka na kitita cha shilingi laki saba(700000).

Naye mshindi wa pili kwa upande wa wanaume ni kikundi cha Kikumba  ambao walizawadiwa kiasi cha shilingi laki saba(700000)na upande wa wanawake nafasi ya pili ilikamatwa na kikundi cha warumona ambao walizawadiwa shilingi laki sita(600000).

Mshindi wa tatu hadi nae kwa wanaume ambaye ni kikundi cha Mwakaye ameondoka na kitita cha shilingi laki nne na nusu(450000)na washindi wanne hadi wa kumi walizawadiwa kifuta jacho cha shilingi laki tatu ambao ni vikundi vya (4)Katonga A(5)Umoja(6)Kalalangabo(7)Tanganyika stars(8)Sigunga(9)Balimi(Bushabani).

Kwa upande wanawake msindi wa tatu alipewa kitita cha shilingi laki tatu na mshindi wa nne hadi wa kumi walipewa kifuta jasho cha shilingi laki mbili na nusu(250000)kila kikundi ambao ni(4)Lembo)(5)Tanganyika(6)Fasta star(7)Mama Kikongwe(8)Kirasa(9)Mwamgongo(10)Upendo.