Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), Mhandisi Ronald Lwakatare akitoa taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha uliopita kwa kamati ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kamati hiyo pia ilifanya ziara ya kujionea miundombinu ya mradi wa mabasi hayo.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), Mhandisi Ronald Lwakatare (katikati) akifafanua jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa iliyofanya ziara ya kutembelea miundombinu ya mradi huo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa kamati hiyo, Bw, Jasson Rweikiza na mjumbe wa kamati hiyo, Bw. Emmanuel Papian (kushoto).
Basi na sehemu ya barabara ya mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) eneo la Sokoine Drive jijini Dar es salaam.