Thursday, November 12, 2015

BARUA YA WAZI KWA RAIS DR. JOHN POMBE MAGUFULI KUTOKA KWA MDAU WA USALAMA BARABARAN


BARUA YA WAZI KWA RAIS DR. JOHN POMBE MAGUFULI KUTOKA KWA MDAU WA USALAMA BARABARAN
Ndugu Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, 

Nachukua fursa hii kukupongeza kwa kuchaguliwa kuliongoza taifa letu la Tanzania kama Rais wa awamu ya tano.

Nianze barua yangu kwa kugusia changamoto ya ajali nchini. Ajali limekuwa ni tatizo sugu licha ya juhudi mbalimbali zinazofanywa na wadau mbalimbali kutoka taasisi binafsi na serikali. Ni hivi karibuni ripoti ya mwenendo wa ajali za barabarani imetolewa na Tanzania ikishika nafasi ya tano kwa kuwa na matukio mengi ya ajali barani Afrika. 

Ajali hizi zimekuwa zikipoteza raslimali nyingi sana ikiwepo raslimali watu na raslimali mali. Hii ni vita inayohitaji juhudi za wadau mbalimbali kupambana nayo kama ilivyo mapambano dhidi ya Ukimwi, Malaria, Rushwa n.k

Barua yangu inalenga kutoa ushuri katika mambo 16 ya fuatayo;
1.      Katika kuunda wizara zako, napendekeza kuwe na "Wizara ya Ujenzi ya Majiji" hii iwe maalumu katika kuratibu shughuli zote zinazohusu Masterplan ya Majiji yetu mbalimbali yaliyopo na yanayochipukia.Hii ijihusishe katika ujenzi wa barabara za kisasa kwaajiri ya miaka 50 ijayo.
2.      Miji yote mikubwa ijengwe "Ring roads" ili kupunguza misongamano ya magari isiyo ya lazima
3.      Taa za barabarani zibadilishwe kwa kuweka taa zinazohesabu kutoka 10 mpaka 0, ili dereva aweze kukadiria kama anaweza kuwahi taa pasipo kuleta madhara kama ilivyosasa.
4.      Maeneo ya Makazi au maeneo ya watu wengi kama Buguruni, Manzese, Mbezi ya Kimara, Mwenge na maeneo ya Mashuleni kama ilivyo Makongo na kwingineko kama maeneo haya yajengwe madaraja "FOOT -BRIDGES" ili watu wavuke maeneo hayo, tofauti na ilivyosasa watu wanavuka barabara huku mioyo wameshika mkononi.
5.      Kwa faida ya wengi, nyumba zilizokaribu na miundo mbinu ya barabara watafutiwe mbadala na kufidiwa kwa haki kulingana na thamani ya eneo lake kwa ajili ya kupisha barabara zinazofaidisha wengi.
6.      Vivuko maalumu viwepo kwenye barabara kwa ajili ya kuwapisha walemavu wanapotaka kuvuka barabara hizo.
7.      Kuwekwe Kamera barabara za mijini ili kuwawezesha askari wa barabarani wafanye kazi wakiwa ofisini badala ya kusimama juani kama ilivyo sasa.
8.      Kushughulikiwa swala la rushwa sehemu za mizani, Checkpoints ambapo ulegevu wa usimamazi wa sheria umesababisha barabara nyingi kuharibika kutokana na magari kuzidisha mizigo na kuruhusiwa kupita kwa urahisi maeneo hayo.
9.      Serikali na taasisi zake kufungua milango ili kuweza Kushirikiana kwa ukaribu na wadau wa Usalama barabarani kama ilivyo "Dereva Makini Tanzania", "Road Safety Ambassadors Tanzania (RSA)", "Amend Tanzania", Safespeed Foundation n.k
10.  Kumekuwa na malalamiko kutoka kwa watumiaji wa barabara mpya za mradi wa mwendo kasi kuwa ni nyembamba hususan maeneo ya Kimara, tunashauri usanifu wa barabara zingine katika miradi kama hii izingatie upana unaobaki kati ya gari moja na jingine ili kuondoa ajali zinazoweza kuzuilika.
11.  Tunakuomba ushughulikie kwa ukaribu sana tatizo ambalo linaonekana kuwa sugu linalo leta ajali za kuumiza sana, Malori yenye makontena (Semi-Trailers) kudondokea na kuyafunika magari madogo.
12.  Tunaomba pia liangaliwe upya swala la alama na blocks zinazowekwa kwenye makutano ya barabara na reli ikibidi kuwe na automatic blocks kuzuia magari treni inaposogea karibia na makutano haya.
13.  Tunakuomba uumalize mgogoro sugu uliopo kati ya madereva, serikali na waajiri kwakuwa tunaoumia ni sisi maskini tunaotegemea usafiri wa mabasi kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
14.  Wachungulie kwa ukaribu wauza vipuli vya mabasi na ubora wa vifaa hivyo kupitia TBS kwa kuwa kuna watu wanapiga deal kwenye maisha ya watu.
15.  Yamulike makampuni ya mabasi na ya bima kuhakikisha wanakata bima kubwa kwaajiri ya mabasi yao, ili wahanga wa ajali walipwe stahili zao kama inavyostahili kuliko kama ilivyosasa kampuni ya bima inapiga deal na mmiliki wa mabasi.
16.  Angalia uwezekano pia wakuingiza technolojia ya Usafiri wa majini kupitia fukwe zetu mbalimbali za Bahari ya Hindi,Ziwa Nyasa,Victoria,Tanganyika na Rukwa yaani "AMPHIBIOUS BUS TECHNOLOGY" ambayo italiongezea taifa pesa kupitia Utalii wa majini "Ocean Tourism"

KWA HESHIMA NA TAADHIMA NAWASILISHA

Peter George Nzunda,
Mdau wa Usalama barabarani
+255687 966 638