Tuesday, July 28, 2015

“PEDRO” ALMASI INAYOKARIBIA KUOKOTWA KWENYE TIFUTIFU



"PEDRO" ALMASI INAYOKARIBIA KUOKOTWA KWENYE TIFUTIFU

pedro-rodriguez-9

"PEDRO" ALMASI INAYOKARIBIA KUOKOTWA KWENYE TIFUTIFU

Nimezaliwa Monduli nimekulia Monduli na ninaishi Monduli..! Sikuwahi
kuona bendera ya vyama vingine zaidi ya chama fulani chenye rangi
wanayovaa Norwich City…! ila leo kila nyumba ina bendera zenye rangi
ya msimbazi….! Mimi sielewi haya mambo, ndio maana nakimbilia kwenye
soka maana huku hakuna kupepesa macho..! huwezi ukakatwa endapo una
kiwango kama cha Mwashiuya..! lini umeona jina la cr7 linakatwa?
Singano je? Mpira unachezwa uwanjani bana na hauitaji vyeti.! hapa
kiwango tuu ndo kitakuweka juu.! unajua leo leo tunazungumzia nini?
Kaa na ukurasa huu hadi mwisho ili tuwe pamoja…!

Yeye, Lionel Messi, Andres Iniesta, Xavi Hernandez, Gerald Pique,
Sergio Busquest na Dani Alves ndo wachezaji pekee kuchukua "treble"
mara mbili wakiwa na klabu ya Barcelona. Msimu wa mwaka 2009-10
alikuwa mchezaji wa kwanza kufunga katika mashindano 6 tofauti
yanayotambulika na Fifa, pia aliwahi kuwafunga Deportivo de la Coruna
goli la umbali wa karibu mita 40, nazani hili ndo goli lake bora
kabisa kuwahi kutokea….! Ana kasi sana, pia ana chembe chembe za
ukorofi kwa mbali japokuwa amekulia La Masia na kila siku alikuwa
akiwaona Xav na Iniesta wakijifunza nidhamu..! ila bado sio mzuri
kwenye nidhamu.

"MVP" ilikuwa ni "Combination" hatari sana duniani, inawezekana dunia
ya soka ilizani hakutatokea "Partneship" nyingine kali kama hiyo la
hasha..! ujio wa Sanchez, Christian Tello na Isaac Cuenca ulianza
kuhatarisha maisha ya Pedro Rodriguez mapema kabisa kabla ya 2012,
achilia mbali majeruhi pia ujio wa Suarez na Neymar ndo kama ulikuwa
msumari wa mwisho utosini mwa Pedro, kijana anaevaa jezi namba 7
mgongoni mwake, "nafahamu kuwa Pedro anataka kuondoka klabuni, hii ni
kutokana na kutopata nafasi ya kucheza muda mwingi. lakini huyu ni
mchezaji wa kimataifa, ameshinda makombe mengi akiwa hapa Barcelona..
…. tena akiwa na wachezaji watatu bora pembeni, natumaini atabaki
kwa sababu ni mchezaji makini na ana kiwango bora, kama ataondoka
atatuachia pengo kubwa katika kikosi chetu" anamaliza Pique.

Najua inauma sana kwa mashabiki wa Barca ila hamna jinsi, hakuna
marefu yasiyo na ncha, japokuwa bado yupo Spain ila usishangae muda
wowote akapanda ndege kuelekea visiwa vya Uingereza kwenda kuwaburuza
mabeki wa Epl..! Ni hisia kali sana za uchungu watakazozipata
mashabiki wa Barca kama hili litatimia ila hakuna jinsi acha aende
akafanye makubwa kama Cesc na Sanchez ambao wote walitupiwa virago
pale Camp Nou.

Kwa pale Barcelona endapo huyu jamaa ataondoka bila shaka watamisi
vitu vingi kutoka kwake kwani tunapozungumzia washambuliaji
wanaokimbia sana uwanjani sizani kama yupo anaemzidi Pedro..! kuna
wakati alikuwa anaitwa jina la utani "Pedro Roadrunner"..! kukimbia
kwake kulikuwa kunawafanya mabeki na walinda milango kufanya makosa
ambayo yanazigharimu timu zao. Pia Pedro baada ya kukosa nafasi mara
karibu zote kwenye kikosi kinachoanza amegeuka kuwa "super sub", bila
shaka unakumbuka hata mechi ya fainali dhidi ya Juve aliingia dakika
za jioni kabisa na kutoa pasi ya goli la mwisho…!

Msimu uliopita alifunga magoli 11 huku akitoa assist 6 pekee. Ni wazi
haya yote yanatokea kutokana na "Combination" ya MSN kufanya vyema..!
ila kwa upande wa Barca bado hawana "sub" nzuri kwa sasa pale mbele
zaidi ya Pedro, anaweza kucheza kama winga au mshambuliaji na kutokana
na kasi na umri wake basi ni wazi Barca walipaswa kumpa angalau dakika
20 za mwisho kila mechi ili aweze kupata faraja na matumaini pale Camp
Nou..! endapo mmojawapo kati ya wale MSN atapata majeraha au
"suspension" ni wazi Barca watamkumbuka winga huyu anaejua
"ku-dribble" na kupiga mashuti yenye macho…!

Endapo atatua mojawapo ya klabu za Epl bila shaka Pedro atageuka
Almasi iliyokuwa inakanyagwa mchangani, kumbuka sio mara ya kwanza
Barca kuwanyanyasa wachezaji wenye viwango, Sanchez, Fabregas na Villa
ni baadhi ya wanandinga ambao wamekwenda kugeuka lulu kule
walipokwenda baada ya kuonekana wapuuzi pale Camp Nou, naamini atakuwa
winga au mshambuliaji mzuri huko aendako.! kila lakheri japokuwa
inauma sana hasa kwa mashabiki wa Barca kuondokewa na Pedro lakini
hakuna jinsi acha aende akatafute changamoto pengine kuliko kusugua
bench pale Catalunya.

Tchaoooo