Thursday, July 30, 2015

NEC yaongeza muda wa SIKU NNE kujiandikisha Dar..ZOEZI LITAENDELEA MWISHO jumanne agosti 4



NEC yaongeza muda wa SIKU NNE kujiandikisha Dar..ZOEZI LITAENDELEA MWISHO jumanne agosti 4
11811510_1065246360159936_8140805964569826706_n
Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu Damian Lubuva .

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema kuwa inaongeza muda wa siku nne tu wa kuandikisha wapiga kura kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam.

 Hii inamaanisha kuwa zoezi hilo ambalo lilikuwa linaisha ijumaa ya kesho julai 31, litaendelea hadi jumanne agosti 4
Akiongea na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu Damian Lubuva amesema kuwa hataweza kuongeza muda wa zaidi ya siku nne kwa kuwa ratiba zitaingiliana.

Aidha, Jaji Mstaafu Lubuva amesema mpaka sasa watu zaidi ya milioni 18 wameandikishwa katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa njia ya mfumo wa kielektroniki BVR kwa nchi nzima.