Friday, August 22, 2014

MATUKIO : SEHEMU ZA KWENDA MKAZI WA DAR ES SALAAM KATIKA WEEKEND YAKO




MATUKIO : SEHEMU ZA KWENDA MKAZI WA DAR ES SALAAM KATIKA WEEKEND YAKO Kwa mkazi wa Dar es salaam na maeneo ya jirani weekend yako unaweza kuitumia kwa sehemu mbili tofauti na kwa wakati tofauti kwa ajili ya kumtukuza mungu.

Usiku wa ijumaa ya leo tarehe 22 August katika kanisa la Living Water Makuti Kawe kuanzia saa tatu usiku na kuendelea, kutakuwa na usiku wa kusifu ambao umeandaliwa na kundi la uimbaji la Soul Music Gospel Tanzania. ambapo kiingilio ni shilingi elfu tano (5000). pia kutakuwa na waimbaji mbalimbali kama The SMG International, Living Water, Paul Clement, Mellody Ndichu (Kenya), The Barikey, Bomby Johnson, Glorious Worship Team, Doxaz, Calvaly Band na wengi mbalimbali.



Wakati hayo yakiwa usiku wa ijumaa ya leo, kwa upande mwingine ni siku ya jumapili ambapo kutakuwa na sherehe ya kutimiza mwaka mmoja wa mkakati wa Yesu Okoa Mitaa (YOM) ambao unafanywa na wanaharakati wa Gospel Hip Hop.

Sherehe hiyo itafanyika katika kanisa la DCT lililopo maeneo ya Tabata shule karibu na Dar West kuanzia saa nane mchana na kuendelea na itakuwa ni bure, ambapo wanaharakati wa Gospel Hip Hop watamsifu Mungu kama vile Rungu la Yesu, Apostel Bashando, Gazuko ambaye yupo kwenye kinyang'anyiro cha tuzo za AFRICA GOSPEL MUSIC AWARDS , Mophat, Peter Sombasomba, Elandre, DCT Worship Team na wengine zaidi angalia kwenye Tangazo hapo chini.

Uwamuzi ni kwako msomaji wetu ambae upo Dar es salaam na maeneo ya jirani kuchukua hatua ya kwenda kuunga na watu wengine mbalimbali katika kumtukuza Mungu.