Friday, July 24, 2015

Mbunge wa Karatu, Mchungaji Israel Natse aachana na Ubunge baada ya miaka 5 amesema anarudia kazi yake ya Uchungaji katika Kanisa la KKKT.




Mbunge wa Karatu, Mchungaji Israel Natse aachana na Ubunge baada ya miaka 5 amesema anarudia kazi yake ya Uchungaji katika Kanisa la KKKT.

Mbunge wa Karatu kwa tiketi ya CHADEMA, Mchungaji Israel Natse, amejitoa rasmi katika siasa na kurudia kazi yake ya uchungaji katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini.


Akizungumza na mwandishi wa NIPASHE kwa njia ya simu ya kiganjani jana, alisema kwa mujibu wa makubaliano yake na chama, walimwomba agombee kipindi kimoja tu, kwa hivyo sasa anampisha mwingine.

"Mimi ninarudi kwenye kazi yangu ya uchungaji naachana na siasa, huu ndiyo wito wangu nilioitiwa na mungu wa uchungaji"

Akinukuliwa na gazeti la MWANANCHI alisema, "Jumatano nitawaaga rasmi wananchi wangu, binafsi niliombwa na Dk Slaa kugombea jimbo hili kwa miaka mitano"

Chanzo: 
NIPASHE.