Friday, July 24, 2015

BHALALUSESA ASISITIZA UMUHIMU WA UMAHIRI KATIKA TEHAMA


BHALALUSESA ASISITIZA UMUHIMU WA UMAHIRI KATIKA TEHAMA IMG_8834
Kiongozi wa kitaifa wa mradi wa CFIT, Prof. Ralph Masenge akimkaribisha mgeni rasmi Kaimu Kamishina wa Elimu, Benjamin Kulwa (hayupo pichani) kufungua kongamano linalohusu upitiaji wa waraka wa mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu linalofanyika mjini Bagamoyo.


IMG_8915
Kaimu Kamishina wa Elimu, Benjamin Kulwa akisoma hotuba kwa niaba ya Kamishina wa Elimu, Profesa Eustella Bhalusesa wakati akifungua rasmi kongamano linalohusu upitiaji wa waraka wa mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu linalofanyika mjini Bagamoyo. Kulia ni Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph.
Na Mwandishi wetu, Bagamoyo
KAMISHINA wa Elimu, Profesa Eustella Bhalalusesa amesisitiza haja ya kuhakikisha kwamba viwango vya umahiri vya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu nchini vinakua vya juu kukidhi haja ya matumizi ya kufundishia na kujifunza nchini.
Alitoa kauli hiyo mjini hapa wakati akifungua kongamano linalohusu upitiaji wa waraka wa mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu.
Katika hotuba yake iliyosomwa na Kaimu Kamishina wa Elimu, Benjamin Kulwa alisema kwamba changamoto ya Tehama inaonekana wazi katika matumizi yake na hivyo wakufunzi lazima wawe mahiri.
"Duniani kote, sekta ya uchumi, fani mbalimbali, taasisi na hata mifumo ya maisha yanategemea sana matumizi ya Tehama kwa sasa. Kadhalika, maendeleo makubwa katika Tehama yamebadili namna mambo yanavyofanyika,รข€ alisema.
Alisema kwa kuhakikisha kwamba kuna maendeleo ya kutosha ni vyema walimu kuwa na umahiri unaotakiwa kwani Tehama inachangamoto nyingi zinazotakiwa kuangaliwa ili kuweza kuitumia ipasavyo kuleta mabadiliko katika jamiii.
Aliwataka washiriki kuhakikisha kwamba wanapitia muswada huo kwa makini na kujazia maeneo yote ambayo wataalamu wameshindwa kumaliza na kusaidia kuweka mtaala huo vyema kwa mafunzo.
Kongamano hilo ambalo ni sehemu ya mradi wa kuimarisha uelewa kwa wanafunzi na wakufunzi vyuo vya walimu ili kuboresha matumizi ya Tehama katika mafunzo hasa masomo ya sayansi limeshirikisha wataalamu mbalimbali na kuendeshwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa kushirikiana na watu wa China.
Alisema kwamba serikali inatambua kuwa Tehama inaweza kutumika vyema katika kubadili na kuboresha mfumo wa elimu Tanzania.
Aidha alisema Sera mpya ya elimu na mafunzo ya mwaka 2014 inatambua umuhimu wa Tehama katika kuboresha viwango vya elimu nchini Tanzania.
Alisema moja ya malengo ya sera ni kuonesha mahitaji halisi ya Tehama nchini katika upande wa wataalamu na vifaa ili kufanikisha utoaji wa elimu hata ya masafa katika ngazi zote.
Kongamano hilo ni moja ya mradi wa China Funds in Trust Project (CFIT) wa UNESCO na serikali ya China wenye lengo la kusaidia serikali ya Tanzania kuimarisha umahiri wa wakufunzi na walimu kwa kuwawezesha kujua tehama na kuitumia.
Mradi huo umelenga kuongeza uwezo wa vyuo vya walimu na teknolojia ya kisasa ya Tehama na vifaa vyake ili kusaidia kujifunza na kufunza.
Ingawa kwa sasa vyuo vinavyofanyiwa kazi na mradi huo vipo viwili vipo vingine vinane vinavyofunza walimu wa sayansi na hesabu vitaingizwa.
IMG_8909 IMG_8842
Pichani juu na chini ni washiriki wa kongamano linalohusu upitiaji wa waraka wa mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu wakati kongamano hilo likiendelea mjini Bagamoyo.
IMG_8843 IMG_8831
Kiongozi wa kitaifa wa mradi wa CFIT, Prof. Ralph Masenge (kushoto) akijadili jambo na mgeni rasmi Kaimu Kamishina wa Elimu, Benjamin Kulwa (katikati). Kulia ni Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph.
IMG_8826
Kiongozi wa kitaifa wa mradi wa CFIT, Prof. Ralph Masenge (kulia), akifurahi jambo na Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph (katikati) pamoja na Mratibu wa kitaifa wa mradi wa CFIT kutoka UNESCO, Faith Shayo (kushoto) mara baada ya kufunguliwa rasmi kwa kongamano linalohusu upitiaji wa waraka wa mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu.
IMG_8928
Mgeni rasmi Kaimu Kamishina wa Elimu, Benjamin Kulwa (walioketi wa pili kushoto) katika picha ya pamoja na washiriki wa warsha hiyo inayomalizika leo mjini Bagamoyo.