Sunday, August 10, 2014

Mh. Zitto atikisa Mwidau CUP Pangani



Mh. Zitto atikisa Mwidau CUP Pangani
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema), amesema hatua ya Tanzania kutofanya vizuri katika michenoa ya kimataifa ni kukosekana misingi imara wa kuinua vipaji kuanzia ngazi ya chini.

Hayo alisema leo mjini Pangani alipokuwa akizindua mashindano ya Mwidau CUP, ambapo asema hatua ya Tanzania kutoka patupu katika mashindano ya Olimpiki ni kielelezo tosha cha kuhitaji maandalizi ya kina.

"Nchi yetu haijapata bahati ya kufanya vizuri kwenye michezo kwani hivi juzi timu zetu zilikuwa katika michuano ya Olimpiki nchini Scotland lakini hatukupata medani hata moja.

"Wiki iliyopita tulikuwa Maputo Msumbiji timu yetu ya Taifa imetolewa kwenye mashindano ya Mataifa huru. Tanzania kwa mara ya mwisho ilishiriki mashindano ya mataifa huru tangu mwaka 1980. Hatujawahi kushiriki tena na sababu kubwa tumesahau kujenga vipaji," alisema Zitto.

Alisema ni vigumu kumnenepesha ng'ombe siku ya moja ya mnada ila kinachotakiwa ni juhudi kama zilizonzishwa na Mbunge wa Viti Maalum Amina Mwidau (CUF), kuibua vipaji kuanzia ngazi za chini. Alimtaka mbunge huyo kuhakikisha mashindani yajayo yakuwa na timu za chini ya miaka 17 ambazo zinatasaidia katika kuibua vipaji zaidi.

"Hii itatusaidia kuwajua watoto bado wadogo kwani hapa Pangani wapo kina Ulimwengu na kina Mbwana Samatta. Ninatoa wito kwa mashirika ya umma kuwa na timu zao kama ilivyokuwa miaka ya nyuma kwani hii itasaidia kuinua soka letu na hata michezo mingine katika Taifa letu," alisema.

Kwa upande wake mbunge wa Viti Maalum, Amina Mwidau (CUF), alisema mashindano ya mwaka huu yamekuwa na maboresho makubwa ambapo mshindi wa kwanza atapata zawadi ya Sh 500,000 wa pili 400,000, wa tatu Sh 300,000 huku mshindi wa nne akijinyakulia Sh 100,000.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema), akizungumza na wananchi katika uzinduzi wa mashindano ya soka ya Mwidau CUP leo mjini Pangani.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema), akiingia uwanjani kuzindua mashindano ya Mwidau CUP .Kushoto ni mdahamini wa mashindano hayo ambaye pia ni mbunge wa Viti Maalum Amina Mwidau.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema), akiwa ameshika ngao ya hisani ambayo iliwania katika mchezo wa ufunguzi wa Mwidau CUP, ambapo timu ya Torino iliibamiza APL ya Mwera bado 2-0.