Nchini Tanzania mtindo wa matumizi ya Dola ya Marekani katika ulipaji huduma na bidhaa unaendelea kushamiri, jambo ambalo lina lalamikiwa na wananchi kuwa ni kinyume cha sheria.
Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania ya (BoT) ya mwaka 2006, inabainisha kuwa shilingi ya Tanzania ndiyo fedha halali kwa malipo ya bidhaa na huduma ikiwamo hotelini, maduka makubwa, nyumba za kupanga na huduma nyinginezo.
Mwandishi wetu Faraja Sendegeya ameandaa taarifa hii kuhusu matumizi ya dola katika biashara ya nyumba za kupanga Jijini Dar Es Salaam.