Immaculate Makilika –MAELEZO ARUSHA
Rais wa Shirikisho la Ujerumani amesema Serikali yake iko tayari kushirikiana na Mahakama ya Afrika katika utendaji kazi wake ili kusaidia kutoa huduma iliyokusudiwa kwa walengwa.
Rais huyo ameyasema hayo leo alipotembelea Mahakama ya Afrika iliyopo mjini Arusha, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya siku sita nchini na kusema kuwa angependa kuona utawala wa sheria ambao unaozingatia demokrasia unafuatwa na kuheshimiwa.
Aidha, Rais Ghauck ameipongeza mahakama hiyo kwa weledi wake na hatua nzuri waliyofikia huku akitolea mfano kesi iliyosikilizwa mwaka 2014 huko Adis Ababa, Sudan.
'Tunaunga mkono maendeleo pia tungependa kuendelea kushirikiana nanyi, msisite kutuomba msaada alisema Rais Gauck'.
Naye kwa upande wake Jaji Mkuu wa Mahakama ya Afrika Augustino Ramadhani alisema Serikali ya Ujerumani imekua na ushirikaiano mzuri na Mahakama hiyo kwani ilisaidia pia katika ujenzi wake.
Hata hivyo jaji Ramadhani amesema wamemuomba Rais wa Ujerumani asaidie kujenga mahakama ya Afrika ya Mashariki, ombi ambalo Rais huyo amesema atalishughulikia kushirikiana na viongozi aliongozana nao.
Aidha, Jaji Ramadhani amesema kuwa uwepo wa Mahakama hii Afrika ni jambo la kujivunia kwani itaweza kusaidia matatizo ya waafrika wote kutoka sehemu mbalimbali.