Monday, December 29, 2014

MH. LOWASSA AMTEMBELEA SUKWA SAID SUKWA,ZANZIBAR


MH. LOWASSA AMTEMBELEA SUKWA SAID SUKWA,ZANZIBAR
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (kulia) akisalimiana na Katibu mkuu wa Zamani wa Umoja wa Vijana wa CCM, Sukwa Said Sukwa alipomtembelea kwa ajili ya kumjulia hali, nyumbani kwake eneo la Mpendae, mjini Unguja jana. Mh Lowassa alikuwa Zanzibar kwa mapumziko ya kusherekea skukuu ya Krismasi.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (kulia) akiwa katika mazungumzo na Katibu mkuu wa Zamani wa Umoja wa Vijana wa CCM, Sukwa Said Sukwa alipomtembelea nyumbani kwake eneo la Mpendae, mjini Unguja jana. Mh. Lowassa alikuwa Zanzibar kwa mapumziko ya kusherekea sikukuu ya Krismasi. Kushoto ni Mke wa Sukwa, Fatma Mussa.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwa katika picha ya pamoja na familia ya Katibu wa Zamani wa Umoja wa Vijana wa CCM, Sukwa Said Sukwa alipomtembelea nyumbani kwake eneo la Mpendae, mjini Unguja jana.