JESHI la Polisi mkoani              Mwanza linamshikilia askari wake WP Fatuma wa Kituo cha              Polisi Igogo wilayani Nyamagana kwa kosa la kumjeruhi              mtumishi wake wa ndani kwa mkumkata vidole vyake vinne vya              mkono wa kulia kwa panga, akimtuhumu kumwibia Deki ya Video              nyumbani kwake. 
        Tukio hilo la kujeruhiwa              kijana Steven Magessa (18), lilitokea Oktoba 20 mwaka huu              katika kijiji cha Magange Mugumu wilayani Serengeti mkoani              Mara nyumbani kwao kijana huyo aliyekuwa amekimbilia huko              baada ya kudaiwa kumwibia mwajili wake nyumbani eneo la              Igogo.
                AKIONYESHA NAMNA              ALIVYOJERUHIWA NA MAMA HUYO
        Akizungumza na waandishi              wa habari kijana huyo alieleza kuwa kufanya kazi kwa askari              huyo kulikuja mara baada ya askari huyo kumfuata kijijini na              kumuomba ridhaa ya wazazi wa kijana huyo kuambatana naye              jijini Mwanza ili kumsaidia kazi za nyumbani ambapo              walikubaliana malipo ya kiasi cha Sh 50,000/= kila mwezi              jambo ambalo askari huyo alilikiuka na kushindwa              kulitekeleza kwa muda wa miezi sita bila kumlipa mshahara.
        
        

 
