Waziri                wa Afya Mh. Seif Rashid akiongea na Wauguzi wa Hospitali                teule ya Mkoa wa Temeke, Wafanyakazi wa Ghetto Radio ya                Sibuka Fm pamoja na wadau mbalimbali wakati wa uzinduzi                Rasmi wa Radio hiyo, ambayo lengo lake ni kuwakomboa                vijana wa Mtaani pamoja na vipindi vingine vya kuelimisha                Jamii na Burudani, Pia amewashukuru kwa kutoa msaada wa                vifaa mbalimbali ambavyo vitasaidia katika Hospitali hiyo                leo Tarehe 1.11.2014
           Mkurugenzi wa Sibuka George                Ndagali akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ghetto                Radio ya Sibuka Fm iliyo fanyika katika  katika Hosipitali                Teule ya Mkoa wa Temeke Ambapo Ghetto Radio Imeweza                kufunguliwa Rasmi Katika Mkoa huo nakuweza kutoa Msaada                Vifaa Mbalimbali pamoja na Madawa Ambavyo Vyote kwa ujumla                vimegharimu kiasi Cha Shilingi Milioni sita na Laki sita.
           Mkurugenzi wa Ghetto Radio Matt                Brouwer akizungumza neno wakati wa uzinduzi wa Ghetto                Radio ya Sibuka Fm Ambapo Bw.Brouwer Alisema kuwa Ghetto                Radio ilianzishwa nchini Kenya Miaka Sita iliyopita                nakuweza kuwasaidia vijana mbalimbali Hivyo wameweza                kuingia Nchini Tanzania Ilikuendeleza kuwapa vijana Fursa                Na elimu INayo Tolewa na Kituo Hicho Kwa Hapa Nchini
          Mganga Mkuu wa Hospitali teule                ya Mkoa wa Temeke Amaani K. Malima akitoa neno la                Shukurani kwa Timu nzima ya Ghetto Radio ya Sibuka Fm kwa                kufanya uzinduzi wa Radio yao katika Hospitali hiyo pia                kutoa Msaada wa vitu mbalimbali vitakavyo saidia katika                eneo hilo.
           Meneja wa Ghetto Radio ya                Sibuka Fm  Edward  Lukaka  akitoa maelezo machache ya                malengo ya Radio hiyo pia kueleza mikakati ya kuendelea                kutoa msaada wa vifaa mbalimbali vya tiba katika Vituo                zaidi vya Afya.
           Mkurugenzi wa kituo cha afya                cha Iran Nchini Tanzania Dkt. Farhad Arjomandi                akiwashukuru Ghetto Radio ya Sibuka FM kwa kuanzisha Kituo                hicho pia na wao wametoa vifaa vya matibabu kwa ajili ya                kushiriki uzinduzi huo wa Radio
           Mwenyekiti wa Red Cross Mkoa wa                Dar es salaam Leonard Masonu  akitoa neno la Shukurani
          Hivi ni Baadhi ya vitu ambavyo                vimetolewa na Ghetto Radio ya Sibuka Fm katika Hospitali                teule ya Mkoa wa Temeke wakati wa uzinduzi Rasmi wa Radio                hiyo
            
           Waziri wa Afya Mh. Seif Rashid                akikabidhiwa Rasmi msaada wa Vifaa na Vitu mbalimbali                vitakavyo tumika katika Hospitali teule ya Mkoa wa Temeke                kutoka kwa Ghetto Radio ya Sibuka Fm
          Waziri wa Afya Mh. Seif Rashid kushoto Akishukuru kwa vifaa hivyo.
 Baadhi ya Wadau mbalimbali                walioshiriki katika Sherehe hiyo ya Uzinduzi Rasmi wa                Ghetto Radio ya Sibuka Fm
           Baadhi ya Wauguzi wakiwa katika                uzinduzi huo Rasmi wa Ghetto Radio ya Sibuka Fm
           Wafanyakazi wa Ghetto Radio ya                Sibuka Fm pamoja na wadau mbalimbali wakijiandaa kuelekea                kutoa Msaada wa vitu mbalimbali katika vyumba vya wagonjwa
            Wakiwa wanaelekea Wodini
           Kulia ni Mkurugenzi wa Sibuka                George Ndagali akiwa katika Wodi ya watoto kukabidhi                zawadi za watoto na mama zao, katikati ni Mwanamuziki                Mkongwe wa Bongo Flava Juma Nature ambaye ni Balozi wa                Ghetto Radio ya Sibuka Fm
          Balozi wa Ghetto Radio ya Sibuka Fm Juma Nature akiwa anatandika Shuka moja wapo katika Wodi ya watoto kuashiria kukabidhi mashuka hayo.
Baadhi                ya Timu ya wafanyakazi wa Ghetto Radio ya Sibuka Fm
         
