Sunday, October 19, 2014

Vikao vya Kamati za Kudumu za Bunge kuanza Jijini Dar es Salaam Jumatatu



Vikao vya Kamati za Kudumu za Bunge kuanza Jijini Dar es Salaam Jumatatu
Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Thomas Kashililah anawatangazia Waheshimiwa Wabunge wote wa Bunge la Jamhuri kuwa Vikao vya Kamati za Kudumu za Bunge vitaanza Jijini Dar es Salaam Jumatatu Oktoba 20,  2014. 

Kwa tangazo hili waheshimiwa Wabunge wote mnaombwa kuwasili Dar es Salaam siku ya Jumapili tarehe 19 Oktoba 2014.

Kamati za Bunge katika vikao hivi vitakavyodumu hadi tarehe 2 Novemba 2014 zitapokea na kujadili pamoja na mambo mengine Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi wa mwaka 2014, Kukagua miradi mbalimbali, kutembelea Mamlaka ya Bandari, Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo na kujadili Sheria ya VAT katika muktadha wa Sekta ya Elimu nchini. Pia zitapokea taarifa kuhusu Sheria ya mazingira inavyotekelezwa katika migodi ya Buzwagi, Geita, Bulyankulu, na North Mara, pamoja na kuijadili kwa ujumla taarifa ya CAG kuhusu ukaguzi wa Hesabu za Serikali Kuu na mashirika ya umma kwa mwaka 2013.

Aidha kutakuwa na maoni ya wadau kuhusu muswada ya Sheria ya Baraza la Vijana wa mwaka 2013 na kupokea taarifa kuhusu migogoro ya mipaka kati ya Hifadhi za Taifa za Saadani, Manyara, Tarangire, Mikumi, Ngorongoro, Ruaha na vijiji vinavyopakana na Hifadhi hizo.

Imetolewa na Ofisi ya Bunge,
Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na
Uhusiano wa Kimataifa,
Dar es Salaam,

18 Oktoba 2014