Friday, October 31, 2014

MHE. PINDI CHANA AFUNGUA KIKAO CHA HALMASHAURI KUU YA UMATI TAIFA


MHE. PINDI CHANA AFUNGUA KIKAO CHA HALMASHAURI KUU YA UMATI TAIFA
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mhe. Pindi H. Chana (Mb.)(katikati) akifuatilia igizo kuhusu kuanzishwa kwa UMATI, mafanikio na changamoto za hutoaji huduma. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa UMATI Bi. Lulu Ng'wanakilala, Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto Bw. Benidect Misani, Mwenyekiti wa UMATI Bibi Rose Wasira na kulia ni Makamu wa Mwenyekiti wa UMATI Bw. Charles Mngodo.
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mhe. Pindi H. Chana akiteta jambo na mmoja wa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya UMATI Taifa ambaye alipata fursa ya kupima afya yake kama sehemu ya huduma zilizotolewa na UMATI sanjari na mkutano katika ukumbi wa Regency Park Hotel jijini Dar es salaam tarehe 30/10/2014.