VYOMBO vya habari zatakiwa kuepuka kupotosha umma juu ya mchakato mzima wa bunge la katiba lililomalizika jana mjini Dodoma.
Kauli hiyo imetolewa leo katika viwanja vya kanisa la Rc Mshindo na mbunge wa jimbo la kalenga Godfrey Mgimwa wakati akichangia kiasi cha Tsh milioni 1.5 wakati wa harambee ya kuichangia radio Maria .
Alisema kuwa iwapo vyombo vya habari zitatumika vibaya kuna uwezekano wa Taifa kuingia katika machafuko kama zilizo nje nyingine na kama vyombo vya habari vitafanya kazi yake kwa kuzingatia misingi ya maadili jamii itaunganishwa na vyombo hivyo.
" Radio Maria ni moja kati ya radio ambazo nimekuwa nikizifuatilia toka nikiwa mdogo na nimekuwa nikipenda zaidi jinsi radio hiyo inavyofanya shughuli zake na mbali ya kufanya kazi ya kueneza injili bado imekuwa msaada mkubwa katika kuelimisha umma……. Hivyo rai yangu kwa radio maria ni kuona inaendelea hivyo hivyo na ikiwezekana kuandaa vipindi kwa ajili ya elimu kwa umma juu ya katiba mpya "
Alisema kuwa wajumbe wa bunge la katiba wametimiza kazi yao ambayo umma ulitegemea kutoka kwa wajumbe hao hivyo kazi iliyobaki ni ya wananchi kucha kuipitisha katiba hiyo mwaka 2016 na kuwa kwa wakati huu ni vema vyombo vya habari kuendelea kutoa elimu kwa umma juu ya kazi nzuri iliyofanywa na bunge hilo la katiba .
Hata hivyo alisema ni vema watanzania kuepukana na watu wachache wasiolitakia mema Taifa ambao wanataka kuona nchi haitawaliki kwa kutaka maandamano yasio na tija kwa jamii.
Mgimwa alisema kuwa njia pekee ya kuepukana na viongozi wasio litakia mema taifa ni pale ambapo vyombo vya habari vitakapoweka msimamo wa uzalendo kwa kuepuka kuwa sehemu ya kuhamasisha kuvunjika kwa amani nchini.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya harambee hiyo Bw Pascal Bella akishukuru kwa mchango huo wa mbunge Mgimwa alisema kuwa mbali ya kuwa mbunge huyo ni wa jimbo la kalenga ila amekuwa msaada mkubwa kwa kufanikisha zoezi hilo la kuichangia radio hiyo.
Bella alisema kuwa kila mwaka na kila wakati wadau wa Radio maria wamekuwa na utaratibu wa kuichangia radio hiyo ambayo uendeshaji wake unategemea michango kutoka kwa wadau mbali mbali na kuwa kwa mwaka huu mkoa wa Iringa pekee unataraji kuchangia zaidi ya Tsh milioni 30