Saturday, October 04, 2014

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AHUDHURIA KONGAMANO LA BIASHARA LA KIMATAIFA KWA NCHI ZA AFRIKA JIJINI DUBAI, FARME ZA KIARABU



MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AHUDHURIA KONGAMANO LA BIASHARA LA KIMATAIFA KWA NCHI ZA AFRIKA JIJINI DUBAI, FARME ZA KIARABU
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika majadiliano kuhusu utengamano wa Afrika na Fursa za biashara na Uwekezaji Katibu na Jumuiya ya Afrika Mashariki, Balozi Richard Sezibera, wakati wakihojiwa na Mwandishi wa habari wa Kimataifa na Mkurugenzi wa Kampuni ya 'Eddo Media', Mark Eddo (kushoto).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania < dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika majadiliano kuhusu utengamano wa Afrika na Fursa za biashara na Uwekezaji, na baadhi ya viongozi, Katibu Jumuiya ya Afrika Mashariki, Balozi Richard Sezibera (katika) na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Ghana, Hanna Tetteh, wakati wakihojiwa na Mwandishi wa habari wa Kimataifa na Mkurugenzi wa Kampuni ya 'Eddo Media', Mark Eddo (kushoto).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (wa nne kutoka kulia) akijumuika na baadhi ya viongozi wakati alipohudhuria Mkutano wa GBF, uliofanyika kwenye Hoteli ya Atlantis jijini Dubai.
Baadhi ya Washiriki wa kongamano hilo kutoka Tanzania, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Nehemiah Mchechu (wa tatu kutoka kulia) akijadiliana jambo na Prof. Ahmada Ktahib kutoka Tume ya Utalii Zanzibar wakati walipohudhuria mkutano huo uliofanyika katika Hoteli ya Atlantis nchini Dubai.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya Viongozi na wawekezaji baada ya kumalizika kwa Kongamano hilo. Picha na OMR