Saturday, October 04, 2014

EFM kukutana na wasikilizaji wake kupitia Tamasha la Muziki Mnene



EFM kukutana na wasikilizaji wake kupitia Tamasha la Muziki Mnene
 Meneja Uhusiano wa Radio 93.7 EFM,Kanky Mwaigomole (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam leo,wakati akizungumzia kuwepo kwa Tamasha la "Muziki Mnene" lenye dhumuni la Radio hiyo kukutana na kuwashukuru wasikilizaji wake katika maeneo mbali mbali jijini Dar,kwa namna walivyoipikea Radio hilo na kuwa nayo pamoja hadi sasa.Katika Tamasha hilo la Muziki Mnene ambapo safari hii litafanyika Oktoba 4,2014 Ukonga Magereza.Wengine pichani ni Mhariri Mkuu wa Radio hiyo,Samira Kiango (kulia) na Afisa Uhusiani wa Radio hiyo,Lydia Charles Moyo.
 Mhariri Mkuu wa Radio 93.7 EFM,Samira Kiango (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya namna Tamasha hilo litakavyokuwa likifanyika.Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Radio 93.7 EFM,Kanky Mwaigomole.
Mmoja wa Watangazaji wa Radio 93.7 EFM kupitia kipindi cha Genge,Pennyl Mungilwa akifanya mambo yake kwenye kipindi chake hicho.