Saturday, October 04, 2014

ANGALIA PICHA: BAWACHA WALIPOANDAMANA KUELEKEA IKULU, HALIMA MDEE AKAMATWA NA POLISI



ANGALIA PICHA: BAWACHA WALIPOANDAMANA KUELEKEA IKULU, HALIMA MDEE AKAMATWA NA POLISI


 Mwenyekiti  wa BAWACHA ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Kawe kupitia CHADEMA Halima Mdee akiwa katika maandamano akiwaongoza wanawake wenzake kuelekea Ikulu kumpelekea ujumbe Rais Jakaya Kikwete kwamba hasikubali kuweka saini Rasimu mpya iliyopitishwa juzi mjini Dodoma, maandamano hayo kabla hayajafika mbali walitawanywa na jeshi la polisi lililotumia maji ya kuwasha pamoja na kupigwa kwa waandamanaji na kumshika mwenyekiti huyo Halima Mdee pamoja na wafuasi wake na kupelekwa polisi Osterbay leo.

 Polisi  wakimpandisha Halima mdee kwenye gari la polisi leo 






 
Mfuasi wa chadema akishikiliwa na polisi na kupelekwa katika gari la polisi
 


 

Halima Mdee akiwa ndani ya gari la polisi pamoja na wafuasi wa chadema wakipelekwa katika kituo cha polisi cha Osterbay.
 
Halima mdee akizozana  na polisi mara baada ya kuingizwa kwenye gari
Wafuasi wa chadema wakimueleza polisi madai yao wakiwa nje ya kituo cha polisi cha Osterbay wakidai kwenda kwa wanaohusika kutuoni hapo kwa ajili ya kumtoa mwenyekiti wao Halima Mndee
 
 
Wafuasi wa chadema wakilalamika  kwa polisi
 
Kituo cha polisi cha Osterbay kilikuwa na ulinzi wa kutosha na hakuruhusiwa mtu yeyote kuingia kituoni hapo
 
Polisi wa Osterbay wakizuia gari kupitia 
 
Wakina mama wa chadema wakifika katika eneo la polisi Osterbay
 
 
Viongozi wa chadema wakiomba kuruhusiwa kupita polisi ya Osterbay