Thursday, December 10, 2015

MHUSIKA WA TATU WA MASHAMBULIZI YA PARIS ATAMBULIWA


MHUSIKA WA TATU WA MASHAMBULIZI YA PARIS ATAMBULIWA
Manuel VallsImage copyrightepa
Image captionWaziri mkuu wa Ufaransa Manuel Valls asema mshukiwa watatu wa mashambulio ya Bataclan ametambuliwa
Polisi nchini Ufaransa wamemtambua mtu wa tatu aliehusika katika mashambulizi ya Bataclan wakati wa mfulurizo wa mashambulizi ya Paris , alisema waziri mkuu wa Ufaransa Manuel Valls.


Bw Valls hakumtaja mtu huyo, lakini hakutofautiana na taarifa zilizomuelezea kama raia wa Ufaransa Foued Mohamed-Aggad, mwenye umri wa miaka 23, kutoka Strasbourg.
Watu 90 waliuawa katika eneo la Bataclan katika shambulizi la mwezi uliopita.
Foued mohames aggadImage copyrightAFP
Image captionFoued Mohamed Aggad anaaminiwa kupata mafunzo ya itikadi kali nchini Syria
Watu wote watatu waliofanya mashambulizi kwenye ukumbi huo wa tamasha wa Bataclan walikua wamevalia mabomu ya kujitolea muhanga wamethibitishwa kuwa na uraia wa Ufaransa.
Washambuliaji wengine walioshiriki katika uratibu wa mashambulizi hayo ya mjini Paris ya tarehe 13 Novemba yaliyowaua jumla ya watu 130 hawajatambuliwa bado kuhusu iwapo ni raia wa Ufaransa ama ni Wabelgiji wenye itikadi kali.
Mohamed-Aggad aliripotiwa kusafiri kutoka Syria mwishoni mwa mwaka 2013 kama mmoja wa kundi la vijana waliopata mafunzo ya itikadi kali kutoka Strasbourg lililomjumuisha pia kaka yake .
Makundi kadhaa baadae yalikamatwa yalipokua yakirejea Ufaransa mwaka. Inaaminiwa kwamba wakati huo Mohamed-Aggad alibakia nchini Syria.
Alitambuliwa wiki iliopita na polisi bada ya kuchukua sampuli za vinasaba (DNA) vilivyowiana na vile vya familia yake.
BBC.