Thursday, December 10, 2015

WATU WANNE WANAOSADIKIWA KUWA MAJAMBAZI YAPORA MIL 80 TANGA


WATU WANNE WANAOSADIKIWA KUWA MAJAMBAZI YAPORA MIL 80 TANGA

Watu wanne wanaosadikiwa kuwa majambazi wamevamia nyumbani kwa mwenyekiti wa kikundi cha kuweka na kukopa kinachojulikana kwa jina la Tuvoka chenye makao yake makuu eneo la Amboni jijini Tanga kisha kudaiwa kupora fedha zaidi ya shilingi milioni 80 ambazo inadaiwa kuwa ni makusanyo ya wanachama wa kikundi hicho kwa muda wa wiki nzima.

Wakizungumza katika nyumba ya mwenyekiti huyo anayedaiwa kuvamiwa kisha kuporwa fedha hizo majira ya saa tisa alfajiri, viongozi, mashuhuda na wajumbe wa kikundi cha Tuvoka wamesema watu hao waliokuwa wamefunika nyuso zao na vitambaa vyeusi wanadaiwa kuwa walivamia majira ya saa tisa afajiri kisha kuingia katika chumba cha mwenyekiti huyo na kumuamuru kuwa awaoneshe mahali fedha hizo ameziweka.

Kwa upande wake katibu wa kikundi hicho Monica Monela akifafanua kuhusu fedha hizo amesema wajumbe wa kikundi hicho wamegawanyika katika sehemu kuu mbili ambapo sehemu ya kwanza walikuwa wameweka fedha kwa mwenyekiti zaidi ya shilingi milioni 43 huku sehemu ya pili waliweka shilingi milioni 42 ambazo kila mwishini mwa 

Mwaka wanagawana faida.

Kufuatia hatua hiyo kamanda wa polisi mkoani Tanga Bwana Zubeir Mwombeji akizungumza kwa njia ya simu amesema taarifa hizo hana na ameshangazwa kwa viongozi wa kikundi hicho kuweka shilingi milioni 80 nyumbani hatua ambayo amesema jeshi lake litafanya uchunguzi wa sula hilo.

Chanzo: ITV