Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mawaziri mbali mbali wakati alipowasili katika Ikulu ya Comoro kwa mazungumzo na Rais wa Nchi hiyo Dr. Ikililou Dhoinine jana akiwa katika ziara ya kiserikali.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwa katika mazungumzo na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Comoro Dr.Ikililou Dhoinine Ikulu Mjini Comoro jana,Dk.Shein yupo Comoro kwa ziara ya kiserikali akiwa na ujumbe aliofuatana nao.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Comoro Dr.Ikililou Dhoinine baada ya mazungumzo Ikulu Mjini Comoro jana,akiwa katika ziara ya kiserikali na ujumbe aliofuatana nao.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akiwa na Mke wa Rais wa Jamuri ya Muungano wa Comoro Mama Dhoinine wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Comoro Dr.Ikililou Dhoinine katika viwanja vya Ikulu ya Comoro jana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiteta na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Comoro Dr.Ikililou Dhoinine Ikulu Mjini Comoro jana, wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa kwa ujumbe Serikali ya Mapinduzi ukiwa katika ziara Nchini Comoro.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Rais wa Jamuri ya Muungano wa Comoro Dr.Ikililou Dhoinine wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa kwa ujumbe Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika ziara ya kiserikali nchini Comoro. [Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]