Wednesday, September 17, 2014

NEWS ALERT: ASKARI WA TATU WAJERUHIWA NA MLIPUKO WA BOMU SONGEA


NEWS ALERT: ASKARI WA TATU WAJERUHIWA NA MLIPUKO WA BOMU SONGEA
 Askari Polisi wakiwa eneo la tukio ikiwa ni kuimarisha ulinzi
(Picha Zote na demasho.com)
-------------

ASKARI watatu  wa jeshi la Polisi wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa  wa Ruvuma  (Homso) iliyopo mjini songea Mkoani humo  wakiwa wanapatiwa matibabu ya majeraha ambayo waliyapata baada ya kushambuliwa kwa kitu kinachodhaniwa kuwa ni Bomu la kurushwa kwa mkono.

Tukio hilo limetokea  September 16, 2014 majira ya saa moja na nusu jioni katika kata ya Msufini karibu na daraja la Matarawe, wilayani Songea Mkoani Ruvuma  ambapo watu watatu wasiofahamika walitupa kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu la kutupwa kwa mkono ambalo limetengenezwa kienyeji na kuwajeruhi askari  hao watatu waliokuwa doria.

Askari hao waliojeruhiwa ni  WP. 10399 PC Felista aliyejeruhiwa mguu wa kulia  kwenye unyayo na pajani  ,G. 7351 PC Ramadhani aliye jeruhiwa mguu wa kulia karibu na goti na tumboni upande wa kulia na  G. 5515 pc John aliyepata majeraha katika mguu wa kulia chini ya goti na jeraha dogo tumboni.

Mganga mkuu wa Hospital ya Mkoa wa Ruvuma Dr. Daniel Malekela ameeleza kutoa vipande vya bati na misumari katika majeraha ya askari hao na mpaka sasa wanaendelea na matibabu.

Alisema kufutia hali hiyo Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma linaendelea na uchunguzi  wa kina ili kuwakamata wahusika wa tukio hilo kwa hatua zaidi za kisheria.
 Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Mhe. Saidi Mwambungu kasema  amesikitishwa sana na kitendo hicho cha wahalifu kujeruhi askari tena kwa makusudi na amesema serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi na usalama watahakikisha wanawasaka na kuwakamata.
 Eneo la tukio  likiwa limezungushiwa alama na Jeshi la Polisi.
 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwangu akizungumza jambo na waandishi wa habari katika hoptal ya mkoa wa Ruvuma baada ya kuwatembelea majeruhi hao
 Kamati ya ulinzi na Usalama wakiwa Hospital ya mkoa wa Ruvuma.
 Aliye lala kitandani ni WP ambaye amejeruhiwa akiwa amelazwa katika hospital ya Mkoa wa Ruvuma
 Mganga mkuu wa Hospital ya Mkoa wa Ruvuma Dr Daniel Malekela akizungumza na wandishi wa habari hopitalini hapo.
Askari Ramadhani Ally akiwa anaelezea jinsi mkasa huo ulivowakuta wakiwa kazini