
Viongozi wa Jumuiya ya Watanzania DMV wakati wakimsubiri Rais Jakaya Mrisho Kikwete Jumapili Julai 3, 2014 katika hoteli ya Marriot jijini Washington DC

Viongozi wa Jumuiya ya Watanzania DMV wakati wakimsubiri Rais Jakaya Mrisho Kikwete Jumapili Julai 3, 2014 katika hoteli ya Marriot jijini Washington DC

Viongozi na wanachama wa Jumuiya ya Watanzania DMV wakati wakimsubiri Rais Jakaya Mrisho Kikwete Jumapili Julai 3, 2014 katika hoteli ya Marriot jijini Washington DC

Wajumbe wa Bodi ya Jumuiya ya Watanzania DMV

Rais Kikwete akimsalimia mmoja wa watoto waliokuwepo kumlaki

Rais Kikwete akilakiwa na wanajumuiya

Rais Kikwete, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernad Membe, Balozi wa Tanzania Marekani Mhe Liberata Mulamula na Bi Rose Jairo, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora wakijadiliana jambo meza kuu


Washiriki wa mkutano huo

Wanajumuiya wakiwa wametulia mkutanoni

Wanajumuiya

Wanajumuiya toka kila kona ya DMV na sehemu mbalimbali za Marekani

Sehemu ya viongozi wa Jumuiya na wanajumuiya

Wote wametulia wakifuatilia kinachoendelea

Wanajumuiya

Wanajumuiya

Wanajumuiya

Sehemu ya nyomi ya wanajumuiya

Wanajumuiya pamoja na baadhi ya viongozi
























Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited,Bw Charles Singili akiongea na kunadi bidhaa mpya ya Diaspora Banking ambayo benki hiyo imeanzisha




Mwanajumuiya akiomba ufafanuzi wa maswala kadhaa yanayowasibu

Wanajumuiya wakifurahia jambo

Swali toka kwa mwanajumuiya

Wanajumuiya wakisikilia kwa makini kinachoendelea

Mwanajumuiya akiuliza swali

Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited,Bwa.Charles Singili akifafanua mambo kadhaa kuhusu Diaspora Banking

Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited,Bwa.Charles Singili akiendelea kutoa ufafanuzi

Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited,Bwa.Charles Singili akieleza faida za Diaspora Banking

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC),Julieth Kairuki akiongea

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC),Julieth Kairuki akifafanua jambo

Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV BW Iddi Sandaly akiongea

Rais Kikwete akifafanua jambo. Kushoto ni Mama Salma Kikwete na kulia ni Balozi Mulamula

Mtangazaji wa Clouds FM kipindi cha Power Breakfast Gerald Hand akirekebisha mitambo

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernad Membe akifafanua jambo

Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV BW Iddi Sandaly akimtambulisha Bi Rose Jairo, Kaimu Mkurugenzi wa Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa

Nyomi

Mawziri na wabunge waliohudhuria

Sehemu ya waliohudhuria


Rais Kikwete akihuytubia wanajumuiya wa DMV


Hotuba ikiendelea
--
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewataka Watanzania waishio nje ya nchi na wanaotaka kuona Tanzania inakubali kuanzisha mfumo wa uraia pacha kutumia muda wao kujenga hoja za jambo hilo badala ya kupoteza muda kwenye mijadala ya blogu na kulaumi watu wengine.
Mwisho!
--

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewataka Watanzania waishio nje ya nchi na wanaotaka kuona Tanzania inakubali kuanzisha mfumo wa uraia pacha kutumia muda wao kujenga hoja za jambo hilo badala ya kupoteza muda kwenye mijadala ya blogu na kulaumi watu wengine.
Rais Kikwete amewataka Watanzania hao kusema ili wasikike kwa sababu, kimsingi, hoja ya uraia pacha haina nguvu miongoni mwa Watanzania wanaoishi Tanzania bali hoja hii inatokana zaidi na msukumo wa Watanzania wanaoishi nje ambao kwa bahati mbaya hawafanyi jitihada za kutosha kutetea hoja yao.
Rais Kikwete ameyasema hayo usiku wa Jumamosi, Agosti 2, 2014, wakati alipokutana, akazungumza na kujibu maswali ya Watanzania wanaoishi Marekani, hasa katika maeneo ya jiji la Washington D.C., na majimbo ya Virginia, Maryland, New York na hata California katika mkutano uliofanyika katika Hoteli ya Marriot Washington, mjini Washington D.C..
Rais Kikwete yuko katika ziara ya siku tisa katika Marekani ambako miongoni mwa mambo mengine atahudhuria Mkutano wa Kwanza wa Marekani na Afrika ambao shughuli zake zinaanza leo Jumatatu. Mkutano huo, umeitishwa na Rais Barack Obama wa Marekani na unahudhuriwa na viongozi wa nchi 47 kutoka Afrika.
Rais Kikwete amewaambia Watanzania hao kuacha kupoteza muda kujadili mambo yasiyokuwa na maana na badala yake kuelekeza nguvu zao katika kujenga hoja yenye nguvu zaidi ya uraia pacha, jambo ambalo ni moja ya mambo yatakayojadiliwa katika mchakato wa Katiba mpya.
"Mnashinda kwenye blogu mkijadili mambo ambayo wenzenu nyumbani wana uwezo mkubwa zaidi kuyajadili kuliko nyie. Mnajiingiza katika mambo ambayo sisi nyumbani tuna uwezo mkubwa nayo kuliko nyie. Kwa mambo haya, sisi tunatosha zaidi. Mnaacha kujadili mambo yanayohusu maisha yenu – kama hili la uraia pacha na mnajiingiza katika mambo yasiyowahusu," amesema Rais Kikwete na kuongeza:
"Kwa sasa upo huu mjadala wa uraia pacha ni hoja yenu. Nyie badala ya kushiriki katika mjadala huu kwa njia zote, mnashinda kujadili mambo ambayo hayana maana. Kwanza hoja ya uraia pacha siyo hoja ya watu wengi nyumbani, siyo jambo linalowahusu. Hata rasimu sina uhakika kama mmeisoma vizuri na kujua nini kimependekezwa – lakini hata huo muda hamna. Kazi yenu mnashinda mnajadili mambo yasiyokuwa na maana – nani kavaa nguo fupi, nani kafanya nini, haya ndiyo mambo yanayochukua muda wetu."
Rais Kikwete amesisitiza: "Ushauri wangu ni kwamba tumieni muda wetu kusaidia kusukuma hoja yenu hii muhimu – ambayo kama mnavyojua imeingizwa katika rasimu kwa mapendekezo ya CCM kwa sababu suala hilo halikuwemo katika rasimu ya kwanza."
Mwisho!
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
04 Agosti, 2014