Na Magreth Kinabo – MAELEZO
Rais Jakaya Kikwete amewataka wafanyabiashara nchini kuongeza juhudi za kuongeza ubora zaidi wa bidhaa zao ili ziweze kushindana na zile za nje ya nchi.
Aidha Rais Kikwete amewapongeza washiriki wa maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa kwa kuongeza ubora wa bidhaa ambao kila mwaka kumekuwa na tofauti.
Kauli hiyo imetolewa leo na Rais Kikwete wakati akitembelea leo maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere jijini Dares Salaam.
" Maonesho ya mwaka huu yamepiga hatua kubwa kwani kumekuwepo kwa ongezeko la bidhaa, bidhaa zimefungwa vizuri tukiendelea hivi tunaweza kushindana na bidhaa za kimataifa. Pendekezo langu mimi ni kuendelea kufanya ziwe vizuri zaidi," alisema Rais Kikwete.
Akitembelea banda la Jeshi la M,agereza, Rais Kikwete ambapo alijionea uzalishaji wa bidhaa za kilimo, alilitaka jeshil hilo kutoa elimu kwa wananchi juu ya kilimo bora cha kisasa.
Katika ziara hiyo Rais Kikwete alitembelea mabanda mbalimbali likiwemo la Wakala wa Mafunzo nje ya nchi. Benki Kuu ya Tanzania, Bidhaa za Tanzaniana mengineyo.