Thursday, July 03, 2014

OFISI YA RAIS, TUME YA MIPANGO YAKAGUA MRADI WA MAKAA YA MAWE NGAKA



OFISI YA RAIS, TUME YA MIPANGO YAKAGUA MRADI WA MAKAA YA MAWE NGAKA
Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango (ORTM), Dkt. Philip I. Mpango, (wa tano kutoka kushoto) akikagua Mradi wa Makaa ya Mawe Ngaka. Wengine ni viongozi na maofisa kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango na Shirika la Maendeleo la Taifa – NDC pamoja na wataalam wa kampuni ya TANCOAL inayojishughulisha na uchimbaji wa makaa ya mawe. 
 Viongozi na Maofisa kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango na NDC wakiwa katika picha ya pamoja na wataalam wa Kampuni ya TANCOAL ndani ya mgodi wa makaa ya mawe. Kampuni ya TANCOAL ndiyo inayohusika nauchimbaji wa makaa ya mawe katika Mradi wa Mkaa ya Mawe Ngaka.

 Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango Dkt. Philip I. Mpango (wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na maofisa kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. Kutoka kushoto wengine ni Naibu Katibu Mtendaji Sekta za Uzalishaji Bw. Maduka Paul Kessy, Naibu Katibu Mtendaji anayeshughulika na Huduma za Jamii na Idadi ya Watu,  Bi. Florence Mwanri, pamoja na wachumi kutoka Ofisi ya Rais Tume ya Mipango Bi. Salome Kingdom, Bw. Erasmus Masumbuko na Bw. Andrea Aloyce.
 Viongozi na maofisa kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango na wale wa NDC wakipata maelezo kuhusu mradi wa makaa ya mawe Ngaka kutoka kwa Mtaalam wa Kudhibiti Ubora (Quality Control Superintendent) Bw. Boscow R. Mabena
 Viongozi na maofisa kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango na NDC pamoja na wataalam kutoka TANCOAL wakiwa katika eneo ambalo uchakataji wa makaa ya mawe unafanyika.
 Timu kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango na NDC wakipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Kikundi cha Wanawake cha Mbalawala, Bi. Joyce Haule juu ya matumizi ya makaa ya mawe majumbani. Makaa hayo hutumika majumbani kwa kutumia majiko maalum baada ya kubadilishwa kitaalam na kuwa rafiki kwa matumizi ya majumbani. Mbalawala kinajihusisha na shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwa ni jitihada za kumkwamua mwanamke kiuchumi
 Majiko maalum yanayotumia mkaa uliotokana na makaa ya mawe  kwa ajili ya kupikia majumbani.
Mtaalam wa Kudhibiti Ubora, Bw. Boscow R. Mabena  akitoa maelezo namna ambavyo Coal Briquett Machine (Pichani) hutumika kubadili makaa ya mawe kutoka hali yake ya mwanzo baada ya kuchimbwa na kutengenezwa kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.