Thursday, July 03, 2014

OCD Mbeya Mjini akutana na wananchi wa eneo la Ndongole



OCD Mbeya Mjini akutana na wananchi wa eneo la Ndongole
OCD wa Wilaya ya Mbeya Mjini,Richard Mchomvu amekutana na kuzungumza na wananchi wa Eneo la Ndongole, Wilayani hapo,wakati wakizungumzia juu ya maswala ya uhalifu unaotokea mara kwa mara katika eneo hilo.katika mazungumzo hayo,OCD Richard Mchomvu amesema kuwa kuanzia sasa Jeshi la Polisi litapambana vilivyo na wahalifu waliopo katika maeneo hayo,huku akijipanga kukabiliana vyema na vijana wanao vuta bangi na kuuza madawa ya kulevya katika eneo la makabulini.Wakitoa dukuduku lao,Wananchi hao wamedai kuwa katika eneo hilo watu hubakwa na kuporwa vitu na vibaka.OCD Richard Mchomvu amedokeza juu ya proglam ya Jeshi la Polisi iitwayo{FAMILIA YANGU IKO SALAMA}.Picha na Fadhil Atick.
Kamanda wa Polisi Wilaya ya Mbeya Mjini,OCD Richard Mchomvu akizungumza na wananchi wa  Eneo la Ndongole, Wilayani hapo.
Kamanda huyo akiendelea kupokea taarifa mbali mbali.
Mmoja wa Wakazi wa eneo hilo la Ndongole, Wilayani Mbeya Mjini akitoa dukuduku lake wakati wa Mkutano na OCD wa Wilaya hiyo.
Sehemu ya wananchi.