Wednesday, December 03, 2014

Balozi seif ahitimisha ziara ya siku mbili Mkoa wa Magharibi, Unguja



Balozi seif ahitimisha ziara ya siku mbili Mkoa wa Magharibi, Unguja
Mlezi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Magharibi Kichama ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi amewahakikishia wananchi wa Zanzibar na Tanzania kwamba uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2015 unatarajiwa kuwa wa utulivu na amani. 
Alisema Serikali kupitia vyombo vyake vya dola vitahakikisha kuwa vikundi vya kihuni vinavyoanza kuandaliwa kwa ajili ya kuvuruga uchaguzi huo itapambana navyo kwa nguvu zake zote. 
Balozi Seif Ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alieleza hayo wakati akihutubia Mkutano wa hadhara baada ya kumaliza ziara ya siku mbili ndani ya Mkoa wa Magharibi Kichama akiwa mlezi wa CCM Mkoa huo uliofanyika katika uwanja wa Kwamabata Magogoni. 
Alisema wananchi walio wengi wameshuhudia vitendo vya kihuni vilivyofanywa na vikundi vya Vijana kujaribu kuvuruga zoezi la uchaguzi mdogo wa Jimbo la Bububu mambo ambayo alisema hayatokubalika kutokea tena kwenye uchaguzi Mkuu ujao hapo mwakani. 
Aliwatahadharisha wana CCM na Wananchi wote kujiepusha na wimbi la vikundi vilivyojikubalisha kujiingiza katika vitendo vya ugaidi ambayo kamwe havikubaliki Kitaifa wala Kimataifa. 
Katika Mkutano huo wa hadhara Balozi Seif ambae pia ni Naibu Kamanda wa Taifa wa Umoja wa Vijana wa CCM Tanzania aliwatawadha makamanda wa Vijana wa Majimbo na Wilaya zilizomo Mkoa wa Magharibi Kichama baada ya kuteuliwa na Baraza Kuu la UVCCM.
Mapema asubuhi akizungumza katika Kikao cha Majumuisho ya ziara yake ya siku mbili akiwa mlezi wa CCM wa mkoa wa Magharibi hapo Tawi la CCM Mbweni Balozi Seif aliwataka Viongozi wa kamati za siasa za Matawi hadi Mkoa kutoogopa au kusemwa wakati wanapotekeleza majukumu yao. Akimkaribisha Mlezi wa CCM Mkoa huo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Magharibi Nd. Yussuf Mohd Yussuf aliwaasa wananchi wa Majimbo ya Magogoni na Mtoni
 Mlezi wa CCM Mkoa wa Magharibi Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikagua Jengo la Kituo cha Afya cha Jimbo la Mtoni ambalo lililoanzishwa kwa mchango wa Wananchi na Viongozi waliopita wa jimbo hilo.
 Vijana wa matambuizo wa Umoja wa Vijana wa CCM Jimbo la Mtoni wakifanya vitu vyao wakati wa mkutano wao na Mlezi wa Mkoa wa Magharibi Balozi Seif aliyefanya ziara kukagua maendeleo ya Chama Mkoani humo.
 Mlezi wa CCM Mkoa wa Magharibi Balozi Seif akimkabidhi kadi mwanachama Thuwaiba Jeni Pandu akiwa miongoni mwa wanachama wapya wa CCM na Jumuia zake kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Tawi la CCM Pangawe Jimbo la Fuoni.
Wanachama wapya 50 wa Chama cha Mapinduzi na Jumuia zake wa Jimbo Jimbo la Fuoni wakila kiapo cha utii baada ya kukabidhiwa kadi kwenye mkutano wa hadhara hapo Tawi la CCM Pangawe. Picha na Hassan Issa wa  OMPR – ZNZ.