Thursday, July 03, 2014

Kaimu Katibu Mkuu atembelea Banda la Wizara kwenye Maonesho ya Sabasaba


Kaimu Katibu Mkuu atembelea Banda la Wizara kwenye Maonesho ya Sabasaba
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajabu Gamaha akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili kwenye Banda la Maonesho la Wizara katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere ambako Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanafanyika. Wengine wanaoshuhudia ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bw. Mkumbwa Ally (mwenye suti) na Bw. Mashaka Chikoli, Afisa kutoka Idara ya Sera na Mipango.
Balozi Gamaha akizungumza na Watangazaji  kutoka Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kuhusu umuhimu wa ushiriki wa Wizara kwenye maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa kuwa ni pamoja na  kutoa taarifa kuhusu utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi ambayo imejikita kwenye kukuza biashara, kuvutia watalii na kutangaza fursa za uwekezaji kupitia Balozi za Tanzania nje ya nchi.
 Bw. Chikoli akizungumza na mmoja wa wananchi waliofika kutembelea Banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Balozi Gamaha akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa kutoka Wizarani na Taasisi zilizo chini ya Wizara ambazo ni APRM, AICC na Chuo cha Diplomasia (CFR).Picha na Reginald Philip