Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo amepokea hati za utambulisho kutoka kwa mabalozi wanne wanaoziwakilisha nchi zao hapa.Mabalozi waliowasilisha hati zao leo ikulu jijini Dar es Salaam ni pamoja na Balozi Ismail Salem wa Malaysia,Balozi Georges Aboua wa Cote d'Ivore, Balozi Thony Fred Balza Arismendi wa Venezuela na Balozi Ahmat Awad Sakine wa Chad.Pchani mabalozi hao wakiwasilisha hati zao kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete Huku Mkuu wa Itifaki Balozi Mohamed Maharage Juma(Katikati) akiratubu hafla hiyo.
Mhe.Ismail Salem Balozi wa Malaysia akiwasilisha hati zake kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Katikati ni Mkuu wa Itifaki Balozi Mohamed Maharage Juma.
Mhe.Georges Aboua Balozi wa Cote d'Ivore akiwasilisha hati zake kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Katikati ni Mkuu wa Itifaki Balozi Mohamed Maharage Juma.
Mhe.Thony Fred Balza Arismendi Balozi wa Venezuela akiwaasilisha hati zake kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Katikati ni Mkuu wa Itifaki Balozi Mohamed Maharage Juma.
Mhe Ahmat Awad Sakine Balozi wa Chad akiwasilisha hati zake kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Katikati ni Mkuu wa Itifaki Balozi Mohamed Maharage Juma. Picha na Freddy Maro.