Tuesday, July 01, 2014

Jaji ajitoa kusikiliza rufaa ya Ponda

 

TZ_-Cleric

Kiongozi wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu , Sheikh Ponda Issa Ponda.

Na Mwandishi wetu.

Jaji wa Mahakama ya kuu kanda ya Dar es Salaam Shabani Lila aliyekuwa amepangwa kusikiliza rufaa ya Kiongozi wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu , Sheikh Ponda Issa Ponda, amejitoa kusikiliza rufaa hiyo  kwa maelezo Kuwa dhamira yake inamfanya ajione hawezi kusikiliza rufaa hiyo.

Jaji Lila alitoa uamuzi huo mwishoni mwa wiki ambapo alisema dhamira yake haimtumi kusikiliza rufaa hiyo namba 89/2013 iliyokatwa na Mwomba rufaa (Issah Ponda) dhidi ya jamhuri inayo omba Mahakama Kuu itengue hukumu ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ya Mei 9 Mwaka 2013, ambayo ilimtia hatiani kwa kosa la kuingia kwa jinai Katika Kiwanja Cha Chang'ombe Markaz ambapo ilimfunga Kifungo Cha Mwaka mmoja nje na kumtaka  awe mtunza Amani na raia mwema lakini Agosti Mwaka na alikamatwa na kufunguliwa Kesi ya uchochezi kwa Madai ametenda makosa ya uchochezi wakati Akiwa ndani ya Maandalizi ya hukumu hiyo.

"Kwa Dhamira yangu hainitumi kusikiliza rufaa ya Ponda, nimerudisha jarada la rufaa hii  kwa Jaji Mfawidhi ili aweze kumpanga  jaji mwingine wa kusikiliza …..na pia nimelikataa ombi la Wakili wa Ponda, Juma Nassor lilokuwa linaomba Mahakama hii impange Jaji mmoja atayesikiliza rufaa hiyo ya Ponda na ombi lilonalooamba Mahakama hiyo itoe amri ya Kuzuia Kesi ya uchochezi iliyofunguliwa na Jamhuri dhidi ya Ponda  Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro isimame hadi rufaa iliyokatwa na Ponda Katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, itakaposikilizwa kuamriwa.

Ponda aliwasilisha mahakamani hapo ombi la Kuomba Mahakama hiyo itoe amri ya Kuzuia Kesi ya uchochezi inayomkabili Morogoro ,isiendelee kusikilizwa hadi pale rufaa yake aliyoikata mapema Mwaka Jana ya Kapinga hukumu iliyotolewa Na Mahakama ya Kisutu Mei 9 Mwaka Jana, ambayo ilimtia hatiani Kwa kosa la kuingia Kwa jinai Katika Kiwanja Cha Markas Chang' ombe, ambapo Mahakama hiyo ilimfunga Kifungo Cha nje Cha Mwaka mmoja, lakini Agosti Mwaka Jana, alifikishwa Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro akikabiliwa na Kesi mpya ya uchochezi na kutenda kosa wakati yupo chini ya uangalizi wa Kifungo Cha Mwaka mmoja nje.

Mapema Juni Mwaka huu, Wakili Mwandamizi wa serikali Bernad Kongora aliwasilisha pingamizi la awali mahakamani akiomba Mahakama hiyo itupilie mbali maombi  hayo ya Ponda yanayoomba Mahakama itoe amri ya usikilizwaji wa Kesi ya uchochezi iliyofunguliwa Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro yasitekelezwe hadi rufaa yake itakapotolewa uamuzi kwasababu ombi hilo linalengo ya kuharibu muda wa Mahakama na halina Msingi.