What did you think of the match? And the own goal by Nigerian captain, Joseph Yobo? I think he played well. I also think Enyeama deserves African Footballer of the Year 2014. What do you think?
Monday, June 30, 2014
Super Eagles wayaaga mashindano kwa kutandikwa 2-0 na Ufaransa
What did you think of the match? And the own goal by Nigerian captain, Joseph Yobo? I think he played well. I also think Enyeama deserves African Footballer of the Year 2014. What do you think?
Mtangazaji Regina Mwalekwa Aikimbia Clouds FM, Apata Deal la Nguvu Redio Kubwa
Leo Asubuhi Mtangazaji wa Clouds FM Mwanadada Regina Mwalekwa Ametangaza wazi kwenye kipindi cha Power Breakfast cha Clouds FM kuwa anaacha kazi rasmi katika kituo hicho alichofanya kwa muda mrefu, Regina Mwalekwa aliwashukuru Watangazaji na Mabosi wa Kituo cha Clouds kwa Kumlea Vizuri katika kipindi chote alichokuwa hapo.
Regina Mwalekwa hakusita kusema sababu ya Kuacha kazi kituo hicho ambapo alisema amepata kazi katika Shirika la Utangazaji la BBC.
Raisa ndie Redds Miss Kanda ya Kaskazini
hawa ndio washindi wa redd's miss kanda ya kaskazini kwa mwaka 2014
hawa ni wadhimini wa shindano hilo kutoka minjingu
Lemutuzz nae alikuwemo ndani ya Redd's miss kanda ya kaskazini bila kumsahau mwenyekiti wa Taswa Juma pinto
mkuu wa mkoa wa Arusha pamoja na mkuu wa mkoa wa Manyara waliuthuria katika usiku huo wa kumsaka mrembo wa kanda ya kaskazini ambapo katika shindano hilo warembo wanne wamwanzo watakingia katika kambi ya Redd's miss Tanzania
mh hashimu Lundenga akiwa anatangaza washindi wa tatu bora
watembo wakiwa wameingia ukumbini wakicheza wimbo wa ufunguzi
papa mwandago akimwaga maneno akiwa kama muandaaji mkuu wa shindano hili
hawa ndio warembo walioingia tano bora
waandaji wa shindano hilo wakiwa wamekaa kwa mapozi wakifuatilia shindano. PICHA zote na libeneke la kaskazini blog
NHIF YATETA NA WADAU WAKE WA MKOA WA DAR ES SALAAM
KAGASHEKI CUP 2014: TIMU YA KAGONDO YAITUNGUA BUHEMBE FC BAO 1-0
Timu ya Kagondo FC imejipatia Alama tatu muhimu kwenye Mtanange wao dhidi ya timu ya Buhembe FC leo kwenye Uwanja wa Kaitaba Bukoba Mjini kwenye Michuano ya Kombe la Kagasheki. Bao hilo la pekee lilifungwa na Mchezaji namba tisa Mgongoni Abduratif Khamis katika kipindi cha kwanza dakika 37. Kipindi cha kwanza kilimalizika kwa bao hilo 1-0 na kipindi cha pili timu zote mbili hakuna iliyoziona nyavu za mwezake timu licha ya kushambuliana mara kwa mara. Mwamuzi alipuliza kipenga dakika 90 kumaliza mtanange huo na Timu ya Kagondo FC wakiibuka na ushindi huo wa bao 1-0. Mapema leo Mchana Timu ya Nshambya na Kibeta ziliumana na timu zote mbili zilimaliza mtanange kwa sare ya bila kufungana kwa kutoka 0-0. Kesho Ligi hii inaendelea tena kwa siku ya nne na kutakuwepo na michezo miwili, Mapema ni Nyanga vs Kitendaguro na Jioni saa 10:00 ni Wagonga Nyundo "Ijuganyondo Vs Kahororo".
Kikosi cha Timu ya Kagondo Fc
Kipute kilianza kwa Timu ya Buhembe kwa kasi sana
Kipa wa Kagodo chupuchupu afungwe bao hapa katika kipindi cha pili. Kipindi cha pili hakuna aliyeziona nyavu za mwenzake bao hilo lilidumu mpaka dakika za mwisho
Hatari: Kipa wa Kagondo Fc akidaka mpira wa Kona
Kipindi cha Pili dakika za mwishoni Timu ya Buhembe FC ilipata kona mbili lakini haikuweza kusawazisha bao, licha ya kuliandama lango la wenzao Kagondo Fc.
AJTC BINGWA WA BONANZA LA TISA LA WAANDISHI WA HABARI KANDA YA KASKAZINI
![]() |
| mwenyekiti wa Taswa Taifa Juma Pinto akiwa akiwa anakagua timu ya mpira wa pete kutoka AJTC kabla ya mechi ya fainaili kuchezwa |
![]() |
| washabiki wa timu ya AJTC wakiwa wanashangilia mara baada yakukabidhiwa kombe katika bonanza la Taswa |
Meneja masoko wa Mega trade, Godluck Kway akitoa neno ndani ya bonanza hilo
Mkuu wa matukio ya kanda ya kaskazini Bw. Christ Sarakana kutoka TBL akiongozana na meneja masoko na mauzo wa kampuni ya Mega Trade Investment Godluck Kway kukagua timu ya netball ya chuo cha uandishi wa habari AJTC
kikosi cha timu ya mpira wa miguu kutoka cho cha AJTC
Nahodha wa timu ya mpira wa miguu wa AJTC Bw. Alli Ahmedi akikabidhiwa kombe la ubingwa na Mkuu wa matukio ya kanda ya kaskazini Bw. Christ Sarakana kutoka TBL
Timu za Chuo Cha Uandishi wa Habari Arusha (AJTC) juzi zilitwaa ubingwa katika bonanza la tisa la waandishi wa habari Kanda ya Kaskazini, lililofanyika uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Katika bonanza hilo, ambalo mgeni rasmi alikuwa, Mwenyekiti wa Taswa Taifa, Juma Pinto jumla ya timu 10 zilishiriki na liliandaliwa na Taswa Arusha kwa ushirikiano na kampuni ya Ms Unique.
Timu ya soka ya AJTC ilitwaa ubingwa baada ya kuifunga kwa mikwaju ya penati 5-4 timu ya Radio Sunrise, wakati wasichana wa timu hiyo, waliwashinda timu ya chuo cha uandishi wa habari na maendeleo ya jamii (IMS), magoli 18-5.
Mgeni rasmi Pinto ambaye pia ni Mjumbe wa bodi vya Mamlaka ya hifadhi Ngorongoro alikabidhi vikombe na fedha taslimu, ambapo bingwa wa soka alipewa kikombe, pamoja na fedha taslimu 200,000 na seti ya jezi.
Mshindi wa pili wa soka akipata 100, 000 wakati bingwa wa mpira wa pete alizawadiwa kikombe na fedha taslimu 100, 000 huku mshindi wa pili akikabidhiwa tsh 50, 000.
Katika bonanza hilo, ambalo lilidhaminiwa na kampuni ya bia nchini, (TBL), kampuni ya Megatrade Investment, Mamlaka ya hifadhi Ngorongoro, Cocacola, SBC (T) ltd, AICC, Tanzanite Forever, TANAPA na Alphatel,
Timu zilizoshiriki ni Radio 5, timu ya Arusha One, ORS kutoka mkoa wa Manyara, Salam Club, IMS na Taswa Arusha ambayo iliibuka na ushindi katika kukamata kuku.
Akizungumza katika bonanza hilo, Pinto alipongeza washindi na viongozi wa Taswa Arusha kwa kazi nzuri waliofanya.
"Nachukuwa fursa hii kuwapongeza sana Taswa Arusha kwa kuandaa bonanza hili kwani halifanyiki sehemu nyingine nchini"alisema
Awali Meneja matukio wa TBl, Chris Sarakana aliahidi TBL kuendelea kudhamini bonanza hilo kutokana na kuvutia wanahabari na wakazi wengi wa Arusha.
Meneja masoko wa Mega trade, Godluck Kway aliwapongeza wanahabari kwa kushiriki kwa wingi katika bonanza hilo na kuahidi kuendelea kulidhamini.
Subscribe to:
Posts (Atom)





















