Thursday, November 01, 2012

JB Mpiana kuwasha moto jijini Dar Novemba 30,2012



Mkurugenzi wa Kampuni Mpya ya QS Muhonda J Entertainment, Joseph Muhonga (kulia) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati akitangaza uzinduzi wa Kampuni yake hiyo na Kutangaza ujio wa Mwanamuziki wa Kimataifa kutoka nchini Congo,JB Mpiana ambaye atatumbuiza katika viwanja vya Leaders Jijini Dar es Salaam Novemba 30.Katika onyesho hilo ambalo litasindikizwa na wanamuziki mbali mbali hapa nchini wakiwemo,H-Baba,MB Dog na Ney wa Mitego ambao wapo chini ya lebo ya Kampuni hiyo pia kutafanyika uzinduzi rasmi wa Albamu mpya ya Bendi ya Mashujaa uitwao "Risasi Kidole".Wengine pichani ni Mratibu wa Onyesho hilo,King Dodoo (katikati) na Meneja wa Bendi ya Mashujaa,Martin Sospeter.
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya,Hamis Ramadhan a.k.a H-Baba (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam leo juu ya maandalizi yake ya kufanya shoo jukwaa moja na Mwanamuziki wa Kimataifa kutoka nchini Congo,JB Mpiana ambaye atatumbuiza katika viwanja vya Leaders Jijini Dar es Salaam Novemba 30.