Tuesday, September 11, 2012

MAANDAMANO YA AMANI KWA WAANDISHI WA HABARI IRINGA KUANZA SAA 4




Maandamano ya waandishi wa habari katika mkoa wa Iringa kuanza saa 4kamili asubuhi yakipinga mauaji ya mwandishi na mwenyekiti wa IPC Daudi Mwangosi kutokana na kuuwawa na Polisi wakati akitekeleza majukumu yake ya Habari.

Akiongea na mtandao huu kwa njia ya simu mwenyekiti wa kamati ya maandamano Zulfa amesema kuwa maandamano hayo yataanzia katika ofisi ya IPC jengo la nImuku kuelekea katika barabara za posta, Uhindini, kanisani, mshindo round about,vibanda vya ccm kumalizikia viwanja vya garden Manispaa.

Pia amewataka wanahabari na Wananchi kutoa ushirikiano lakini wafahamu kuwa maandamano haya ni maandamano ya amani na kuwatoa wasiwasi kwani kibali cha maandamano hayo kimekwishatolewa na OCD.