KESHO NI IBADA YA KIPAIMARA KANISA LA KILUTHERI JIJINI LONDON |
Baadhi ya waumini wakishiriki chakula cha Bwana ibada iliyopita. |
Vijana watatu wanatarajia kupata kipaimara jumapili ya kesho katika ibada ya kiswahili kanisa la Kilutheri la Mtakatifu Anne jijini London nchini Uingereza. Ibada hiyo inatarajiwa kuanza majira ya saa nane mchana na kufuatiwa na kipindi cha chakula pamoja kusherehea hatua ya vijana hao kupata kipaimara.
Kwa mujibu wa mchungaji Moses Shonga akitangaza kanisani hapo katika ibada ya mwanzo wa mwezi iliyoambatana na ibada ya chakula cha Bwana, aliwataka waumini waliofika siku hiyo kuwaalika na wengine ili kufika hiyo kesho kwaajili ya ibada hiyo maalum kwa vijana.
Aidha katika ibada iliyopita pia waumini waliofika waliweza kukutana baada ya ibada kujadili maendeleo ya kanisa (mkutano mkuu ulioambatana na taarifa ya fedha) pamoja na namna ya wakazi wa Afrika mashariki wanavyoweza kusaidiana katika mambo mbalimbali ambapo mpaka mwisho wa kikao hicho waumini hao walipitisha mambo mazuri ambayo utekelezaji wake unatarajiwa kuanza jumapili hii.
Chini ni baadhi ya picha za ibada iliyopita ya chakula cha Bwana na mkutano mkuu
|
Mchungaji Moses Shonga akihubiri. |
|
Kijana Lusajo akiimba huku akipiga kinanda. |
|
Baadhi ya waumini waliohudhuria ibada hiyo. |
|
Baadhi ya waumini ibada iliyopita. |
|
Bango likiwa mlangoni mwa kanisa kujuza watu muda wa ibada. |