Friday, January 02, 2015

RAIS KIKWETE AMTEUA DK. MIGHANDA MANYAHI KUWA MWENYEKITI MPYA WA BODI YA TANESCO



RAIS KIKWETE AMTEUA DK. MIGHANDA MANYAHI KUWA MWENYEKITI MPYA WA BODI YA TANESCO
Na Chalila Kibuda
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Dk.Mighanda Manyahi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Kwa taarifa iliyotolewa leo na kwa vyombo vya habari  na kusainiwa na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini ilisema ,kufuatia uteuzi huo,Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter  Muhongo amewateua Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa TANESCO .

Wajumbe wa bodi walioteuliwa ni Kissa Vivian Kilindu,Juma Mkobya,Dk.Haji Semboja,Shabaan Kayungilo,Dk.Mtesigwa Maingu,Bodi Mhegi,Felix Kabodya pamoja na Dk.Nyamajeje Weggoro.

Taarifa hiyo ilisema bodi hiyo imeanza kazi Januari 1 na itaishia Februari 31 Mwaka 2017