Friday, January 02, 2015

SHIRIKISHO LA MCHEZO WA BAO TANZANIA (SHIMBATA) KUMUENZI HAYATI MZEE KAWAWA.



SHIRIKISHO LA MCHEZO WA BAO TANZANIA (SHIMBATA) KUMUENZI HAYATI MZEE KAWAWA.
Na Mdau Sixmund J.B

Shirikisho la mchezo wa Bao nchini (SHIMBATA) nilatarajia kufanya Tamasha kubwa la mchezo huo kwa ajili ya kumuunze aliekuwa mlezi wa mchezo huo hapa nchini Hayati Mzee Rashidi Mfaume Kawawa kama sehemu ya kumbukumbu ya miaka mitano ntangu afariki Dunia.

Tamasha hili ambalo litaudhuriwa na wanafamilia ya Mzee Kawawa wakiwemo watoto wake Mh Vita R. Kawawa Mbunge wa Namtumbo (CCM) na Mh Zainabu R. Kawawa Mbunge viti maalumu (CCM) linatarajiwa kufanyika hapo kesho Tarehe 3/01/2015 katika viwanja vya Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam, mkabala na Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM.

"Tamasha hili ni kubwa na nimahususi kwa kumuenzi Mzee wetu Mlezi wetu ambae pia ni Muhasisi wa Taifa hili Mzee Kawawa, kwani mchango wake kwa maendeleo ya mchezo huu ni mkubwa sana, na pia Mjane wa Hayati Mzee Kwawa atakuja kuungana nasi, yeye atakuja mchana saa sita hadi saa nane.

Nichukuwe nafasi hii kuwaalika watanzania wote, wanahabari na wafadhili mbali mbali wajitokeze kuupa heshma mchezo huu kama sehemu ya kumuenzi Mzee wetu Kawawa". Alisema Rais wa Bao nchini Bw Mandei Likwepa.

Mchezo wa Bao ni moja ya michezo mikongwe hapa nchini na ambao unahistoria kubwa hasa katika ukombozi wa Taifa hili la Tanzania, na umekuwa ukichezwa sana na Hayati Baba wa Taifa Mwl J.K.Nyerere enzi za uhai wake.