Tuesday, September 11, 2012

JK: Katika Ufunguzi Wa Chuo Cha Taifa Cha Ulinzi



 
Rais Jakaya Mrisho  Kikwete akikata utepe kufungua rasmi Chuo cha UIinzi (National Defence College) leo Septemba 10, 2012    Kunduchi jijini Dar es salaam. Kulia kwake  ni  Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange na kushoto kwake ni Mkuu wa Chuo hicho, Meja Jenerali Charles Makalala na kushoto kabisa ni aBalozi wa China nchini Tanzania Mhe. Lu Younqing
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Mkuu wa Chuo cha UIinzi (National Defence College) Meja Jenerali Charles Makalala leo Septemba 10, 2012 baada ya kumkabidhi mfano wa funguo kama ishara ya kufungua rasmi chuo hicho kilichopo Kunduchi jijini Dar es salaam. Kulia ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Mkuu wa Chuo cha UIinzi (National Defence College) Meja Jenerali Charles Makalala  baada ya kufungua rasmi chuo hicho kilichopo   Kunduchi jijini Dar es salaam. Nyuma yao ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe Shamsi Vuai Nahodha anayefuatana na  Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisoma hotuba yake kufungua rasmi Chuo cha UIinzi (National Defence College) kilichoko Kunduchi jijini Dar es salaam, pamoja na kuzindua kozi ya kwanza ya mwaka mmoja. Walioketi karibu yake ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange na Mkuu wa Chuo hicho, Meja Jenerali Charles Makalala
 


                                                          PICHA NA IKULU