Monday, August 06, 2012

WAFANYAKAZI GGM WAMTAKA MKURUGENZI SSRA, AG KAMATI YA BUNGE MAENDELEO YA JAMII KUACHIA NGAZI



Wafanyakazi wa mgodi wa dhahabu wa Geita Gold Mine (GGM) wamemtaka Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti  na Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) Irene Isaka ajiuzulu wadhifa huo kwa kudanganya umma na  kushindwa kushauri vizuri katika utungwaji sheria mpya ya mafao.

Wafanyakazi ambao walipanga kuandamana kwa amani kabla ya jeshi la polisi kutengua kibali  cha maandamano hayo, walisema kuwa wataishinikiza seriakli na kuhakikisha  mabadiliko ya sheria hiyo yanafanyika hata kama watafukuzwa kazi.

Sanjari na tamko hilo pia wametishia kuwa wao na familia zao hawatoshiriki kwenye zoezi la sensa ya watu na makazi endapo serikali na Wabunge hawatakaa kusikilzia kilio chao.

Kauli hiyo ilitolewa na  wafanyakazi katika risala yao iliyosomwa kwa mgeni rasmi na  Katibu wa kamati ya kupinga sheria hiyo,Rogers Luhega juzi kwenye mkutamnom wa hadhjara uliofanyika kwenye uwanja wa Magereza Mjini Geita.

Mgeni rasmi alikuwa ni  Jumuiya ya Wafanyakazi (TUCTA) Wilaya ya Geita , Benjamin Dotto  kuwatambua na kuunga mkono kilio chao.

Alisema TUCTA inaunga mkono malalamiko yao wasfanyakazi  kutokana na sheria hiyo kupitishwa bila kushirikishwa wadau katika sekta binafsi na za umma,hatua ambayo ingeweza kusaidia kutungw a kwa sheria isiyo kandamizi lakini kutokana na kupitishwa kwa sheria hiyo kuna haja ya kulalamikiwa ili  baadhi ya vipengele virekebishwe.

Mkutano huo ulifanyika kwenye uwanja wa magereza mjini Geita, baada ya  Jeshi la polisi kubatilisha kibali cha kufanya maandamano kwa wafanyakazi hao ilichokuwa imekitoa awali ambayo yangefanyika Agosti 4 juzi na badala yake wakatakiwa kufanya mkutano wa hadhara kupinga sheria ya SSRA.

Walidai kuwa wanapinga sheria hiyo kutokana na mikataba yao kutokuwa ya kudumu pamoja na mazingira ya kazi za migodini kuwa hatarishi kwa afya zao kunakochangia wengi kufariki hata kabla yakufikisha umri wa miaka 55 hivyo kuwafanya kutoanufaika wao na familia zao juu ya mafao yao baada ya kuondoka kwenye ajira kwa mujibu wa sheria hiyo ya mafao.


Walisisisitiza kuwa ili kuwaridhisha na ahadi zinazotolewa na Wabunge pamoja na Serikali kupitia SSRA juu ya kilio chao wanataka kuwepo na waraka wa maandishi  kwa kila mwanachama badala ya kuarifiwa kupitia mtandao wa kampuni hatua waliyodai wengi kukosa i kuamini inaweza kuwa ni ahadi hewa.
Juzi  Mkuu wa wilaya ya Geita ,Omari Manzie Mangochie alikiri kusitishwa kwa maandamano hayo akidai kutokuwa na  tija kwa sababu tayari serikali na Bunge  vililikuwa vinalinafanyia kazi madai hayo,hivyo kuwataka kuondoa upotoshaji unaofanywa na baadhi ya watu wachache.

Alisema sheria hiyo ilipitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mujibu  wa sheria na mamlaka lilinayo kikatiba na sheria  hivyo haiwezi kubatilishwa au kufanyiwa marekebisho kwa kufanya maandamano na kuacha kufanya kazi za uzaliashaji badala yake wawe na subira  kwani linafanyiwa kazi.

Hata hivyo Mangochie  alikwenda mbali na kuwatuhumu viongozi wa wafanyakazi hao kuwa wanatafuta umaarufu wa kisiasa, kwaqmba wanaojiita viongozi waa wafanyakazi hao ni viongozi wa CHADEMA wilayani humo.

"Hawa ni wahuni tu, wanatafuta umaarufu wa kisiasa, kwa nini washinikize kuanza maandamano yao kituo cha mabasi badala ya kuanzia kazini kwao,"alihoji DC huyo

Awali Luhega alisema kuwa kuanzaia mandamano hayo kituo cha mabasi kulibasbishwa na wafanyakazi wengi kuishi nje mgodi na wengine wanatoka nje ya wilaya hivyo walipanga kukutana stendi kuandama  kuelekea uwanja wa magereza.

Alidai kuwa polisi walizuia mandamano yao kwa maslahi ya watalawa na Chama cha Mapinduzi(CCM) ili kukandamiza haki ya wafanyakazi.

Alisema hawatakaa kimya hadi hapo serikjali itapoamua kurejesha sheria hiyo bungeni ikajadiliwe upya, kwani kipengele kinacholalamikiwa kiilingizwa kinyemela kwa maslahi ya watu wachache na hakikuwemo wakati muswada huo unajadiliwa nma wabunge.

Aliwataka wabunge wa kmati ya Mazingira na Maendeleo ya jamii ya bunge kuwajibika kwa kujiuzulu ili kulinda heshima zao ikiwa ni pamoja na Mwanasheria Mkuu wa serikali kuridhia kupitishwa kwa sheria hiyo aliyoiita ya kipuuzi na kandamizi kwa wafanyakazi kwqa kuwa hakuna mfanyakazi mwenye uhakika wa kufikisha umri wa miaka 55 kulingana na mazingiara yao ya kazi