Sunday, April 05, 2015

HISTORIA FUPI YA WAKOLONI WALIVYOTUFANYA!




HISTORIA FUPI YA WAKOLONI WALIVYOTUFANYA!


Afrika ya Mashariki ya Kijerumani (au: ya Kidachi) ilikuwa jina la koloni ya Ujerumani huko Afrika ya Mashariki kati ya 1885 hadi 1918/1919.
Eneo lake lilijumlisha nchi za kisasa za Tanzania bara (bila Zanzibar), Burundi na Rwanda. Ilikuwa koloni kubwa kabisa ya Dola la Ujerumani

Juhudi za Karl Peters

Koloni hii ilianzishwa na mfanyabiashara Mjerumani Karl Peters mwaka 1885 kwa niaba ya "Kampuni ya Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki".
Peters aliyewahi kusoma chuo Uingereza aliona wivu juu ya ukoloni wa Uingereza akiamini ya kwamba Ujerumani ungestahili nafasi hiyo pia. Hivyo alianza kudai koloni katika mikutanno akaanzisha "Shirika kwa koloni za Kijerumani" mwaka 1884 iliyokuwa kitangulizi cha kampuni. Shirika hii ilimtuma pamoja na wenzake wawili kwenda Afrika na kutafuta nafasi ya kuanzisha koloni. Peters alifika Zanzibar alipoambiwa na konsuli ya Ujerumani ya kwamba hawezi serikali ya nyumbani haikubali mipango yake. Hivyo alivuka barani akapita kanda la neo la Kizanzibari kwnye pwani na kutembelea machifu na masultani barani.
Hapa alifaulu kushawishi watawala wa Usagara, Nguru, Useguha und Ukami kumpa sahihi kwenye mikataba ya Kijerumani ambayo hawakuelewa. Mikataba hii ilisema ya kwamba mtawala alikabidhi nchi yake pamoja na haki juu ya ardhi na mali yote kwa kampuni.
1885 Peters alirudi Berlin na kuonyesha mikataba yake kwa magazeti na serikali. Chansela Bismarck alikataa akacheka mikataba kama karatasi bila maana. Peters alitumia mbinu akatisha kupeleka mikataba yake kwa mfalme Leopold II wa Ubelgiji aliyekuwa kununua haki zake. Hapa Bismarck aliogopa kilio cha wapenda koloni akakubali kumpa Peters barua ya ulinzi kwa maeneo yalikuwa ya kampuni kufuatana na mikataba

Upanuzi na ugomvi na Zanzibar

Peters na wawakilishi wake walirudi wakaendelea kutafuta machifu waliokuwa tayari kutia saini mikataba yake. Sultani ya Zanzibari alipinga juhudi hizi. Zanzibar ilisimamia pwani la Afrika ya Mashariki na tangu karne watu wa miji ya pwani walikuwa na mawali wa Sultani. Zanzibar ilidai pia utawala ya bara hadi Ziwa Tanganyika na Kongo ingawa hali halisi athira yake haikuenda mbali na njia za misafara ambako ndovu na watumwa walipelekwa pwani. Tarehe 27 Aprili 1885 serikali ya Zanzibar ilituma barua Berlin kupinga kazi na madai ya kampuni na kutangaza maeneo ya ya tanzania ya leo kama milki yake. Iliongeza pia wanajeshi wake barani zilizokuwa chini ya amri ya mwanajeshi mstaafu Mwingereza Matthews. Hapa serikali ya Berlin ilituma kikosi cha manowari kwenda Bahari Hindi.
Mwezi wa Agosti manowari za Kijerumani chini ya amri ya admirali Eduard von Knorr zilifika mbele ya Unguja zikalenga mizinga yao kwa ikulu ya sultani. Akishauriwa na balozi wa Uingereza Sultan Bargadh alipaswa kutoa tamko kuwa "Kutokana na madai tunayopelekewa kwa matishio na Kaisari wa Ujerumani tunatambua ulinzi wa Ujerumani juu ya nchi za Usagara, Ngurow, Useguha, Ukami na juu ya wilaya ya Witu. Mipaka yake itaelezwa baadaye na sisi tunatambua ulinzi wa Kaisari juu ya mahali palipotajwa." [1]. Sultani alipaswa pia kutia sahihi mkataba wa biashara na Ujerumani alipokubali haki nyingi kwa Wajerumani katika milki yake. [2].
Mwaka 1886 Uingereza na Ujerumani walipatana juu ya ugawaji wa Afrika ya Mashariki na tena Sultani alipaswa kukubali. Katika mapatano haya Sultani alibaki na visiwa vya UngujaPembaMafia na funguvisiwa ya Lamu pamoja na kanda la pwani barani lenye upana wa maili 10 kati ya mito Rovuma upande wa Kusini na mto Tana upande wa Kaskazini,halafumiji ya KismayuBarawaMerka na Mogadishu upande wa kaskazini zaidi



Mkataba kati ya Zanzibar na Kampuni juu ya kofo na pwani

Mapatano ya 1886 yaliwapa Wajerumani nafasi ya kuendeleza upanuzi barani nyuma ya kanda la pwani la Kizanzibari na mstari wa mpaka ulichorwa kuanzia mdomo wa mto Umba kupitia mlima Kilimanjaro hadi Ziwa Viktoria. Lakini kwa ajili ya matumizi ya kibiashara swali la mabandari bado lilibaki wazi. Hapo Peters na kampuni yake walianza kujadiliana na Sultani Seyyed Bargash kuhusu utawala wa pwani katika sehemu ya Tanganyika.
Mnamo mwaka 1887 Bargash alikuwa amechoka alitafuta pesa tu kwa ajili yake binafsi alikuwa tayari kukodisha utawala wa kanda la pwani la Tanganyika kwa Wajerumani. Wajerumani walidai kuongezeka haki na Bargash alikufa bila kumaliza mapatano. Lakini mfuasi wake Sultani Seyyed Khalifa aliwapa Wajerumani walichotaka. Tarehe 15 Agosti 1888 wawakilishi wa kampuni ya Kijerumani walifika kwenye mabadari yote ya pwani wakatangaza utawala wao kwa niaba ya sultani.

Vita ya Abushiri na mwisho wa utawala wa Kampuni

Badiliko hili lilisababisha upinzani na hatimaye ghasia ya wenyeji. Vipengele ya mkataba vilisema ya kwamba mali isiyokuwa na hati za kimaandishi haiwezi kutambuliwa. Wenye mali kama mashamba walitakiwa kununua hati kutoka kwa watawala wapya. Hapo Waswahili wa pwani walijisikia walisalitiwa na sultani asiyekuwa na haki kuchukua mali zao na kuzipa kwa wageni wa nje.
Mara baada ya kufika kwa Wajerumani kwenye miji ya pwani ghasia ilianza mjini Pangani na kuenea haraka kote pwani kati ya Tanga na Lindi.
Kampuni ilikuwa na Wajerumani wachache tu walioshindwa kujitetea. Walipaswa kukimbia au wakauawa. Bagamoyo pekee palikuwa na kikosi cha askari kzutoka manowari ikatetewa.
Serikali ya Ujerumani iliona lazima kuingia kati ya kutuma manowari pamoja na askari waliokandamiza ghasia.
Baada ya upinzani wa wenyeji wa pwani mwaka 1889/1890 wakiongozwa na Abushiri na Bwana Heri serikali ya Ujerumani iliamua kutwaa mamlaka kutoka kwa kampuni na kufanya eneo lote kuwa koloni ya Dola la Ujerumani badala ya shirika.

Koloni ya Dola la Ujerumani

Utawala wa Kijerumani ulikwisha katika Vita Kuu ya Dunia ya Kwanza (1914 - 1918) kutokana na uvamizi wa Uingereza na Ubelgiji.
Katika Mkataba wa Versailles mwaka 1919 eneo la koloni ya Kijerumani iligawiwa. Sehemu ya Tanganyika ilikabidhiwa kwa Uingereza na maeneo ya Rwanda na Burundi yaliwekwa chini ya Ubelgiji.



Kwa ujumla, historia au tarehe, ni kumbukumbu ya maisha ya mwanadamu duniani, hasa ile tarehe iliyosajiliwa na kuhifadhiwa katika vitabu, maandishi mbali mbali, na simulizi au hekaya za mapokeo. Ingawa historia iliyobebwa katika simulizi na hekaya huchukuliwa na baadhi kuwa haina nguvu kwa kukosa ithbati ya maandishi, bado hivi ni vyanzo muhimu vya historia. Mara nyingi historia iliyoko katika maandishi huwa imehifadhiwa katika simulizi na hekaya kwa muda mrefu kabla ya kuandikwa.
Hapo kale, bara la Afrika lilishuhudia matukio mengi ya harakati za mwanadamu kuliko mabara mengine ya ulimwengu. Wataalamu wa athari wamegundua athari za binadamu zinazorudi nyuma kufikia hadi miaka milioni minne, na athari za ustaarabu wa Wamisri huko Misri na Wafiniki huko Tunis na sehemu nyenginezo za Afrika ya Kaskazini katika karne ya tisa (9) KK.
Harakati za madola makubwa ya Warumi na Waarabu ziliweza kuonekana kabla ya karne ya nne (4) BK, na Waarabu walianza kuingia Afrika huko Habasha (Ethiopia) tangu karne ya saba (7) BK na kutangaza dini yao na kuieneza katika maeneo mbali mbali ya Afrika pamoja na kuanzisha biashara na ustaarabu na utamaduni na kuimarisha mamlaka zao katika Sudan ya wakati huo tangu karne ya nane 8 ya Kikristo.
Himaya za GhanaMali, na Songhai zilikuwa zikijulikana kwa utajiri wao mkubwa na biashara stawi iliyokuwa ikifanyika wakati huo ya dhahabu na bidhaa nyinginezo. Mwisho wa karne ya 15 BK, himaya ya Songhai ilikuwa na nguvu kuweza kuitia chini ya utawala wake mamlaka ya Mali. Sehemu nyingine za kusini ya Afrika zilikuwa wakati huu hazijulikani sana, na historia yake ilikuwa bado haijasajiliwa.
Baina ya karne ya kwanza KK na karne ya kumi na sita (16) BK Watu waliokuwa wakizungumza lugha ya Kibantu watokao sehemu za Nigeria na Cameroon ya leo, ndio waliokuwa wameenea kwenye sehemu mbali mbali kusini mwa bara la Afrika, wakiwa wameanzisha vijiji, mashamba na mamlaka katika sehemu za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ya leo, za Luba na Mwememutapa, lakini makundi ya wachungaji wanyama walianza kuhamia kusini katika karne za 15 na 16 na kukutana na Wabantu. Ndipo walipoanzisha mamlaka zao za BunyoroBugandaRwanda na Ankole.


Ukoloni

Wazungu walianza kugundua bara la Afrika katika karne ya 15, wakati Wareno walipokuja kwenye fukwe za bara la Afrika kutafuta njia nyepesi na ya amani ya kufikia India, na kuweza kupata nafasi ya kushikilia biashara ya dhahabu na pembe na watumwa ambayo ilikuwa ikiendelea wakati huo katika bara la Afrika. Katika mwaka 1488 Bartolomew Diaz alizunguka rasi ya matumaini mema (cape of good hope), na katika mwaka 1498 Vasco da Gama alifika ufukwe wa Afrika Mashariki na kuendelea mpaka India.
Baada ya hapo, Ureno alianzisha vituo vya biashara Afrika kufuatiwa na WaholanziWaingerezaWafaransa na Wazungu wengineo, na biashara ya Watumwa ikashika kani na kuwa na kasi na nguvu. Wakati huu huu Waturuki walishikilia sehemu za kaskazini ya Afrika na Waomani wakashikilia ufukwe wa Afrika Mashariki. Kati ya 1880 na 1912, Wazungu waliligawanya bara la Afrika baina yao, na nchi zote zikawa chini ya utawala wa Wazungu isipokuwa Liberia na Ethiopia.
Wafaransa wakachukuwa Afrika Magharibi na Kaskazini na kwa hivyo nchi za Afrika Magharibi (Dahomey - sasa Benin), GuineaMaliCote d'IvoireMauritania,NigerSenegal na Upper Volta (sasa Burkina Faso) zilikuwa chini ya utawala wake. Hali kadhalika, Algeria, Tunisia na Morocco zilitawaliwa na wao. Aidha, Wafaransa walitawala TogolandSomalilandMadagascarComoro, na Reunion.
Waingereza nao wakatawala Afrika Mashariki na Kusini, na kuwa sehemu ya Sudan na Somalia, UgandaKenyaTanzania (chini ya jina la Tanganyika), Zanzibar,NyasalandaRhodesiaBechuanalandBasutoland na Swaziland chini ya utawala wao na baada ya kushinda katika vita huko Afrika ya Kusini walitawala Transvaal, Orange Free State, Cape Colony, na Natal, na huko Afrika ya Magharibi walitawala Gambia, Sierra Leone, the Gold Coast, na Nigeria.
Wareno wakachukuwa sehemu ya Guinea, Angola, na Mozambique na sehemu na visiwa fulani fulani huko Afrika ya Magharibi. Wabelgiji wakachukuwa Kongo na Rwanda-Urundi, na Wahispania wakachukuwa sehemu ya Guinea, Spanish Sahara (sasa Sahara ya Magharibi),na Ifni na sehemu fulani za Morocco. Wajerumani nao wakachukuwa Togoland, Cameroon, na baadhi ya nchi katika Afrika ya Magharibi na Afrika ya Mashariki, lakini baada ya vita vya kwanza vya dunia wakanyanganywa. Wataliani wakachukuwa Libya, Eritrea na sehemu ya Somaliland.

Uhuru

Nchi ya kwanza kujitawala wenyewe katika Afrika ni nchi za Afrika ya Kusini zilizojiunga na kujiendesha wao wenyewe katika mwaka 1910. Misri, katika mwaka wa 1922 walikuwa wanajiendesha wenyewe, na Tangier katika mwaka wa 1925. Madola mengi ya Afrika yalianza kupigania uhuru katika miaka ya baina 1950 na 1960, na Wazungu wakasalimu amri na kuanza kutoa uhuru. Libya wakajinyakulia uhuru katika mwaka wa 1951, Eritrea katika mwaka 1952 ikiwa imejiunga na Ethiopia, Morocco katika mwaka wa 1956, na wakarudishiwa Tangier. Katika mwaka huu wa 1956, Sudan na Tunisia vile vile walipata uhuru wao, na Ghana katika mwaka wa 1957, Guinea katika mwaka wa 1958, na vile vile Morocco wakarudishiwa Spanish Morocco.
Katika mwaka wa 1960 Ufaransa ukatoa uhuru kwa Cameroon, the Central African Republic, Chad, Congo (Brazzaville), Cote d'Ivoire, Dahomey (Benin), Gabon, Madagascar, Mali, Mauritania, Niger, Senegal na Upper Volta (Burkina Faso). Vile vile, katika mwaka huu huu wa 1960 Congo (Kinshasa), Nigeria, Somalia, na Togo zikapata uhuru wake, na katika mwaka wa 1961 Sierra Leone na Tanganyika zikapata uhuru, na Afrika ya Kusini ikawa Jamhuri. Katika mwaka wa 1962 Algeria, Burundi, Rwanda, na Uganda zikawa huru, na 1963 zikafuatia Zanzibar, Gambia na Kenya, na katika mwaka wa 1964 Malawi (Nyasaland), na Zambia (Rhodesia ya Kaskazini) zikapata uhuru. Baada ya miaka miwili, katika mwaka wa 1966 Botswana (Bechuanaland)na Lesotho (Basutoland) zikajinyakulia uhuru. Mauritius na Swaziland katika mwaka wa 1968 na vile vile Equitorial Guinea. Uhispania ukairudisha Ifni katika mwaka wa 1969 katika mamlaka ya Morocco.
Aidha, katika mwaka wa 1974 Portuguese Guinea (Guinea-Bissau) ikapata uhuru wake, na katika mwaka wa 1975 Angola, Cape Verde, Mozambique, Sao Tome na Principe zikapata uhuru. Uhispania vile vile ukaitoa Spanish Sahara (Western Sahara) na kuwapa Morocco na Mauritania katika mwaka wa 1976, lakini wananchi wa Sahara wakakataa kuwa chini ya nchi mbili hizi, na kukazuka vita. Mauritania ukaitoa sehemu yake na kuipa Morocco katika mwaka wa 1979, tatizo ambalo mpaka sasa linaendelea baina ya Morocco na Western Sahara, na Umoja wa Mataifa unajaribu kutatua tatizo hili. Waingereza wakawapa uhuru Seychelles katika mwaka wa 1976, na Ufaransa ukatoa uhuru kwa visiwa vya Ngazija (Comoro)
Katika mwaka wa 1977 Djibouti (Afars na Issas) iliyokuwa ikitawaliwa na Wafaransa ikarudi kwa wenyewe. Rhodesia (Zimbabwe) ikapata uhuru katika mwaka wa 1980, na South West Africa, iliyokuwa ikihukumiwa na Afrika ya Kusini ikapata uhuru katika mwaka 1990 na kuitwa Namibia. Ulaya Uingereza ukachukuwa visiwa vya St. Helena na Ascension, na Ufaransa ukaendelea kuhukumu Mayotte na Reunion. Uhispania vile vile ukaendelea kutawala visiwa vya Canary na visiwa viwili vya Ceuta and Melilla, vilivyoko karibu na Morocco vikabakia na Uhispania.