Thursday, April 16, 2015

PSPF NA MAX MALIPO WAUNGANA KUKOMBOA WAJASIRIAMALI



PSPF NA MAX MALIPO WAUNGANA KUKOMBOA WAJASIRIAMALI
Mkurugenzi wa Mfuko wa PSPF, Adam Maingu, akifungua mkutano huo kwa risala fupi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers, Eric Shigongo, akihamasisha kila mmoja kujiwekea akiba kupitia mfuko huo.

Mkurugenzi wa Max Com, akimpongeza Shigongo kwa  jinsi alivyoshawishi kila mmoja kujiunga na mfuko huo.
Naibu Waziri, Juma Nkamia, akitoa hotuba fupi kabla ya kuzindua huduma hiyo.

Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Max Com, Juma Rajab, wakimsikiliza Shigongo.Wadau wakimsikiliza Waziri Nkamia.
Waziri Nkamia (kushoto) akizindua huduma hiyo.  Kulia ni Eric Shigongo.
Hapa ni pongezi  miongoni mwa wahusika baada ya uzinduzi.
Wakurugenzi wakiinua mikono juu kuashiria kuendeleza  mshikamano katika huduma hiyo.Mkurugenzi wa Max Com, Juma Rajab (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers, Eric Shigongo wakibadilishana mawazo.
Shigongo akijaza kadi ya kujiunga na mfuko wa PSPF.Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (Maelezo) Zamaradi Rashid Mfaume Kawawa 'Simba wa Vita' (kushoto) na Mkurugenzi wa PSPF, Adam Maingu, wakipiga makofi baada ya kuguswa na uhamasishaji wa Shigongo kujiunga na mfuko huo.

Mmoja wa wadau akilipia huduma hiyo kwa Wakala wa Max Malipo baada ya kujiunga na mfuko huo.Mjomba Band ikitoa burudani wakati mambo yakiwekwa sawa katika hafla hiyo.
Kiongozi wa Mjomba Band, Mrisho Mpoto, akinogesha mambo kwa waliohudhuria.
MFUKO wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) leo umeanzisha mpango wa kuwawekea akiba wajasiriamali binafsi badala ya utaratibu wa zamani wa kuwawekea akiba waajiriwa peke yao.
Katika mpango huo PSPF wanashirikiana na kampuni inayokuja kasi ya Max Com kupitia huduma yake ya Max Malipo ambapo wachangiaji katika mfuko huo watalipia malipo yao kupitia kampuni hiyo na kupatiwa risiti.
Katika mpango huo uliozinduliwa na Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia, Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers, Eric Shigongo, ambaye alikuwa kama mshawishi kwa wananchi kujiunga na huduma hiyo aliwaasa wajasiriamali  mbalimbali wakiwemo wanasoka, waendesha bodaboda, wavuvi na wengineo kujiwekea akiba kupitia mpango huo.
Shigongo alielezea umuhimu wa kujiwekea akiba na madhara ya kutojiwekea akiba.
(HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS / GPL)