Monday, August 04, 2014

PICHA NA TAARIFA KUTOKA IKULU:RAIS KIKWETE ALIPOKUTANA NA WANAJUMUIYA YA WATANZANIA WA DMV KATIKA MKUTANO WA DIASPORA JIJINI WASHINGTON



PICHA NA TAARIFA KUTOKA IKULU:RAIS KIKWETE ALIPOKUTANA NA WANAJUMUIYA YA WATANZANIA WA DMV KATIKA MKUTANO WA DIASPORA JIJINI WASHINGTON
Viongozi wa Jumuiya ya Watanzania DMV wakati wakimsubiri Rais Jakaya Mrisho Kikwete Jumapili Julai 3, 2014 katika hoteli ya Marriot jijini Washington DC
Viongozi wa Jumuiya ya Watanzania DMV wakati wakimsubiri Rais Jakaya Mrisho Kikwete Jumapili Julai 3, 2014 katika hoteli ya Marriot jijini Washington DC
Viongozi na wanachama wa Jumuiya ya Watanzania DMV wakati wakimsubiri Rais Jakaya Mrisho Kikwete Jumapili Julai 3, 2014 katika hoteli ya Marriot jijini Washington DC
Wajumbe wa Bodi ya Jumuiya ya Watanzania DMV
Rais Kikwete akimsalimia mmoja wa watoto waliokuwepo kumlaki
Rais Kikwete akilakiwa na wanajumuiya
Rais Kikwete, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernad Membe, Balozi wa Tanzania Marekani Mhe Liberata Mulamula na Bi Rose Jairo, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora wakijadiliana jambo meza kuu
Sehemu ya wanajumuiya na wageni toka sehemu mbalimbali wakiwa katika mkutano huo
Washiriki wa mkutano huo
Wanajumuiya wakiwa wametulia mkutanoni
Wanajumuiya
Wanajumuiya toka kila kona ya DMV na sehemu mbalimbali za Marekani
Sehemu ya viongozi wa Jumuiya na wanajumuiya
Wote wametulia wakifuatilia kinachoendelea
Wanajumuiya
Wanajumuiya
Wanajumuiya
Sehemu ya nyomi ya wanajumuiya
Wanajumuiya pamoja na baadhi ya viongozi






Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited,Bw Charles Singili akiongea na kunadi bidhaa mpya ya Diaspora Banking ambayo benki hiyo imeanzisha



Mwanajumuiya akiomba ufafanuzi wa maswala kadhaa yanayowasibu
Wanajumuiya wakifurahia jambo
Swali toka kwa mwanajumuiya
Wanajumuiya wakisikilia kwa makini kinachoendelea
Mwanajumuiya akiuliza swali
Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited,Bwa.Charles Singili akifafanua mambo kadhaa kuhusu Diaspora Banking
Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited,Bwa.Charles Singili akiendelea kutoa ufafanuzi
Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited,Bwa.Charles Singili akieleza faida za Diaspora Banking
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC),Julieth Kairuki akiongea
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC),Julieth Kairuki akifafanua jambo
Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV BW Iddi Sandaly akiongea
Rais Kikwete akifafanua jambo. Kushoto ni Mama Salma Kikwete na kulia ni Balozi Mulamula
Mtangazaji wa Clouds FM kipindi cha Power Breakfast Gerald Hand akirekebisha mitambo
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernad Membe akifafanua jambo
Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV BW Iddi Sandaly akimtambulisha Bi Rose Jairo, Kaimu Mkurugenzi wa Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Nyomi
Mawziri na wabunge waliohudhuria
Sehemu ya waliohudhuria
Rais Kikwete akihuytubia wanajumuiya wa DMV
Hotuba ikiendelea
--

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewataka Watanzania waishio nje ya nchi na wanaotaka kuona Tanzania inakubali kuanzisha mfumo wa uraia pacha kutumia muda wao kujenga hoja za jambo hilo badala ya kupoteza muda kwenye mijadala ya blogu na kulaumi watu wengine.

Rais Kikwete amewataka Watanzania hao kusema ili wasikike kwa sababu, kimsingi, hoja ya uraia pacha haina nguvu miongoni mwa Watanzania wanaoishi Tanzania bali hoja hii inatokana zaidi na msukumo wa Watanzania wanaoishi nje ambao kwa bahati mbaya hawafanyi jitihada za kutosha kutetea hoja yao.

Rais Kikwete ameyasema hayo usiku wa Jumamosi, Agosti 2, 2014, wakati alipokutana, akazungumza na kujibu maswali ya Watanzania wanaoishi Marekani,  hasa katika maeneo ya jiji la Washington D.C., na majimbo ya Virginia, Maryland, New York na hata California katika mkutano uliofanyika katika Hoteli ya Marriot Washington, mjini Washington D.C..

Rais Kikwete yuko katika ziara ya siku tisa katika Marekani ambako miongoni mwa mambo mengine atahudhuria Mkutano wa Kwanza wa Marekani na Afrika ambao shughuli zake zinaanza leo Jumatatu. Mkutano huo, umeitishwa na Rais Barack Obama wa Marekani na unahudhuriwa na viongozi wa nchi 47 kutoka Afrika.

Rais Kikwete amewaambia Watanzania hao kuacha kupoteza muda kujadili mambo yasiyokuwa na maana na badala yake kuelekeza nguvu zao katika kujenga hoja yenye nguvu zaidi ya uraia pacha, jambo ambalo ni moja ya mambo yatakayojadiliwa katika mchakato wa Katiba mpya.

"Mnashinda kwenye blogu mkijadili mambo ambayo wenzenu nyumbani wana uwezo mkubwa zaidi kuyajadili kuliko nyie. Mnajiingiza katika mambo ambayo sisi nyumbani tuna uwezo mkubwa nayo kuliko nyie. Kwa mambo haya, sisi tunatosha zaidi. Mnaacha kujadili mambo yanayohusu maisha yenu – kama hili la uraia pacha  na mnajiingiza katika mambo yasiyowahusu," amesema Rais Kikwete na kuongeza:

"Kwa sasa upo huu mjadala wa uraia pacha  ni hoja yenu. Nyie badala ya kushiriki katika mjadala huu kwa njia zote, mnashinda kujadili mambo ambayo hayana maana. Kwanza hoja ya uraia pacha siyo hoja ya watu wengi nyumbani, siyo jambo linalowahusu. Hata rasimu sina uhakika kama mmeisoma vizuri na kujua nini kimependekezwa – lakini hata huo muda hamna. Kazi yenu mnashinda mnajadili mambo yasiyokuwa na maana – nani kavaa nguo fupi, nani kafanya nini, haya ndiyo mambo yanayochukua muda wetu."

Rais Kikwete amesisitiza: "Ushauri wangu ni kwamba tumieni muda wetu kusaidia kusukuma hoja yenu hii muhimu – ambayo kama mnavyojua imeingizwa katika rasimu kwa mapendekezo ya CCM kwa sababu suala hilo halikuwemo katika rasimu ya kwanza."

Mwisho!

Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
04 Agosti, 2014