Saturday, September 03, 2016

TANESCO WAANZA KUBADILISHA MIUNDOMBINU YA UMEME JIJINI DAR ES SALAAM.



TANESCO WAANZA KUBADILISHA MIUNDOMBINU YA UMEME JIJINI DAR ES SALAAM.
Meneja Mwandamizi wa Usambazaji Umeme wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), ambaye pia ndiye Meneja wa Mradi wa kuimarisha miundombinu ya Umeme, Injinia Theodory Bayona.(katikati), akisimamia kazi hiyo leo Septemba 3, 2016.
Kaimu Meneja Uhusiano wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Leila Muhaji, akizungumza na waandishi wa habari kwenye eneo la mradi 

NA K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID
WAHANDISI, na mafundi wa Shirika la Umeme Nchini Tanzania, (TANESCO), kwa kushirikia na wale wa kampuni za Kijapani za Yachiyo Engineering Co Limited, Takaoka na National Construction Co. Limited, wameanza kazi ya uboreshaji miundombinu ya umeme kwenye kituo kikubwa cha kupooza na kusambaza umeme cha Ubungo jijini Dar es Salaam, imeanza leo Septemba 3, 2016.

Kazi kubwa inayofanyika hivi sasa ni kubadilisha laini kutoka umeme mdogo kwenda umeme mkubwa, lakini pia kubadilisha vifaa vingine muhimu ili kuwezesha usafirishaji umeme uweze kuwafikia watumiaji katika ubora ulio juu.

"Ikumbukwe kwamba, hapa tulikuwa na laini mbili (waya mbili) zilizokuwa na uwezo wa kusafirisha umeme kiasi cha Megawati 120 kila moja, kutoka hapa Ubungo kwenda kituo cha Ilala, lakini kazi inayofanyika sasa, ni kubadili njia hizo (waya za umeme), ambazo zitakuwa na uwezo wa kupitisha kiasi cha umeme wenye Megawati 220 kila moja," Alifafanua Meneja Muandamizi wa Usambazaji Umeme wa Shirika hilo, ambaye pia ndiye Meneja wa wa Mradi wa kuimarisha miundombinu ya Umeme, Injinia Theodory Bayona.

Kwa mantiki hiyo, kazi inayofanyika leo hii itawezesha umeme utakaokuwa ukisafirishwa kutoka hapa Ubungo kwenda Ilala, kuwa na jumla ya Megawati 440 kwa laini zote mbili, tofauti na hapo awali ambapo uwezo wa kusafirisha umeme ulikuwa Megawati 240 tu," Alisema.

Kazi ikikamilika wakazi wa jiji la Dar es Salaam, watakuwa wakipata umeme wa uhakika, na ulio bora, alifafanua Injinia Bayona.

Naye Kaimu Meneja Uhusiano wa Shirika la Umeme Nchini Tanzania, (TANESCO), Leila Muhaji, amewaomba wananchi kuwa wavumilivu katika kipindi hiki ambapo Shirika linafanya juhudi kubwa za kuwapatia umeme wa uhakika wananchi kwa kuimarisha miundombinu yake,.

"Ili kuwawezesha mafundi wetu kufanya kazi katika mazingira salama, tutakuwa tukikata umeme kuanzia leo hii Septemba 3 na umeme utakuwa ukikatika kuanzia saa 2 asubuhi na kurejea saa 11 jioni kwa utaratibu na tarehe kama ifuatavyo; Septemba 3-4, Septemba 10-11, Septemba 17-18, na Septemba 24-25, 2016." Alifafanua Leila, na kuwaomba wananc hi kuwa wavumilivu katika kipindi hiki.

Mradi huu ulioanza Februari 2015 na unaotarajiwa kukamilika Juni 2017 unatekelezwa na Serikali kupitia TANESCO kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) .
Tsutomu Sato, wa kampuni ya Takaoka ya Japan, akiwa kazini
Mafundi wa TANESCO, wakitayarisha nyaya hizo mpya
Fundi wa TANESCO, akifunga kikombe wakati wa kazi ya kubadilisha miundombinu ya kusafirisha umeme kwenye kituo kikuu cha kupooza na kusambaza umeme cha Ubungo, jijini Dar es Salaam
Raphael Mjata, Msimamizi Mkuu wa Njia Kuu za Umeme, akionyesha uwezo wa kituo cha Ubungo cha kupooza umeme wenye kilovolti 132.
Mafundi wa TANESCO na kampuni ya National Construction Company Limited, wakivuta nyaya hizo mpya
Hizi ndio nyaya zitakazofungwa kwenye laini mbili za kusafirisha umeme kutoka kituo cha kupooza na kusafirisha umeme cha Ubungo.
Mhandisi Bayona, akielezea waandishi wa habari mwenendo wa kazi hiyo
Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO makao makuu, Leila Muhaji, na Afisa Uhusiano wa Shirika hilo, Henry Kilasila, wakiwa kazini.
Mhandisi Bayona (kulia), akijadiliana jambo na Wahandisi wenzake, Yasutaka Osawa, (kushoto), ambaye ni mwakilishi katika mradi wa kuboresha umeme jiji la Dar es Salaam, kutoka kampuni ya Takaoka Engineering Co Ltd, na Mhandisi Ahmed Mmingwa, ambaye ni Msimamizi wa Mradi kutoka TANESCO.
Fundi wa TANESCO, akiwa kazini leo Septemba 3, 2016.
 Mwakilishi wa kampuni ya Kijapani ya Yachiyo Engineering Co. Limited, Tamai Masayuki,akizungumza na waandishi wa habari kuhsuu maendeleo ya uboreshaji huo


Wahandisi wakijadiliana jambo
Fundi wa TANESCO akiwa kazini.
Kazi inaendelea 
Meneja Mwandamizi wa Usambazaji Umeme wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), ambaye pia ndiye Meneja wa Mradi wa kuimarisha miundombinu ya Umeme, Injinia Theodory Bayona.(katikati), Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Leila Muhaji, (kulia) na Afisa Habari wa Shirika hilo makao makuu, Henry Kilasila, (wakwanza kushoto) na waandishi wa habari, wakitembelea eneo la mradi mapema leo asubuhi Septemba 3, 2016 ambapo kazi ilianza kwa kasi 
Wafanyakazi wa TANESCO chumba cha ufuatiliaji mwenendo wa umeme (control room) wakiwa akzini.
Chumba cha kufutialia mwenendo wa umeme jijini Dar es Salaam, (Control room), cha TANESCO-Ubungo sub station)