Mwalimu Merina Sekilo aliyenusurika kupigwa na radi wakati akifundisha darasa la kwanza,ambapo wanafunzi 6 walifariki
Mwalimu Veronika Mtes wa shule ya msingi Kibirizi aliyepata mshtuko baada ya tukio la radi akiwa katika hospitali ya Mawenzi mkoa wa Kigoma kwa matibabu.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya mkoa wa Kigoma,Maweni akiongeza na Waandishi wa habari juu ya tukio la radi lililotokea hivi punde na kuuwa watu 8
Na Editha Karlo Karlo wa blog ya jamii,Kigoma
WATU wanane wakiwemo wanafunzi sita na mwalimu wa shule ya msingi kibirizi mmoja pamoja na mtu wa kawaida mkazi wa eneo la Bangwe mjini hapa wamekufa baada ya kupigwa na radi huku wanafunzi wengi 15 wakijeruhiwa na radi hiyo mchana huu.
Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa kigoma(maweni)Dkt Fadhili Kabaya alisema kuwa watu hao walifikwa na mauti hayo kufiatia mvua kubwa zilizonyesha zikiambana na radi zilianza majira ya saa sita mchana.
Dkt Fadhili aliwataja waliokufa katika tukio hilo kuwa ni pamoja na mwalimu wa shule ya msingi kibiriziElinaza Mbwambo(25)mtu mwingine wa kaida ni Forcus Ntahaba(45)mkazi wa eneo la Bangwe mjini hapa.
Aliwataja wanafunzi waliofariki ambao wote ni wa darasa la kwanza kuwa ni Yusuph Ntahoma(8)Hassan Ally(9)Fatuma Sley(7)Zamda Seif(8)Shukranmi Yohana(7) na Warupe Kapupa(10).
Alisema walipokea majeruhi kumi na tano lakini kati yao kumi wametibiwa na kuruhusiwa kurudi nyumba baada ya hali zao kuwa nzuri na watano wamelazwa wanaendelea na matibabu katika hospital ya Mkoa wa Kigoma.
Akisimulia tukio hilo mwalimu aliyekuwa anafundisha darasani Mwalimu Merina Sililo alisema kuwa akiwa darasani akiendelea kufundisha ghafla aliona wingu zito jeusi limetanda hadi akashindwa kuendelea kuandika ubaoni.
''Manyunyu yalianza kidogo kidogo ikaja mvua kubwa na radi pamoja na miungurumo mikali sana iliyopelekea wanafunzi kuanguka ovyo darasa na kuzima na mara niliona moto umetanda katika chumba kuzima cha darasa na mimi nilianguka chini na kupoteza fahamu''alisema mwalimu huyo
Alisema apozinduka alijikuta katika hospital ya Mkoa wa maweni akipatiwa matibabu baada ya kuletwa kwa msaada wa waalimu wenzie.
''Kwakweli ni mungu tu mwenyewe ndo ameninusuru kwani nilirushwa mmara tatu na radi na watoto wote wote darasani walikuwa wananiangukia mimi wengine walikuwa wanakimbia ovyo nje''alisema Mwalimu huyo. (Muro)