Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango, wa Wizara                ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Haji Janabi (katikati) na                Balozi wa Japan nchini, Masaharu Yoshiba (kushoto)                wakikata utepe ikiwa ishara ya makabidhiano ya magari                matano yaliyotolewa na Serikali ya Japan kwa ajili ya                kusaidia Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini. Magari hayo                yamekabidhiwa nje ya Jengo la Wizara hiyo, jijini Dar es                Salaam. Kulia anayepiga makofi ni Mkuu wa Jeshi la                Zimamoto na Uokoaji, Kamishna Jenerali, Thobias                Andengenye. 
                Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango, wa Wizara                ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Haji Janabi akitoa hotuba fupi                kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, kuishukuru                Serikali ya Japan kwa kuisadia wizara yake kupitia Jeshi                la Zimamoto na Uokoaji magari tisa kwa ajili ya kazi ya                kuzima moto na uokoaji nchini. Wa pili kushoto ni Balozi                wa Japan nchini, Masaharu Yoshiba akifuatiwa na Mkuu wa                Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kamishna Jenerali, Thobias                Andengenye. Wa pili kulia ni Kamishna wa Operesheni wa                Jeshi hilo, Rogatus Kipali na Kamishna Msaidizi, Fikiri                Salla. Tukio hilo lilifanyika nje ya Jengo la Wizara hiyo,                jijini Dar es Salaam. 
                Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kamishna                Jenerali, Thobias Andengenye akitoa hotuba fupi ya                kumkaribisha mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya                Sera na Mipango, wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Haji                Janabi ili aweze kuzungumza na baadaye kukabidhiwa magari                matano ya kuzima moto na uokoaji. Magari hayo yametolewa                na Serikali ya Japan kupitia balozi wake nchini, Masaharu                Yoshiba. Tukio hilo la makabidhiano lilifanyika nje ya                Jengo la Wizara hiyo. 
                Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara                ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Lilian Mapfa (kushoto)                akimkabidhi zawadi Balozi wa Japan nchini, Masaharu                Yoshiba, mara baada ya Balozi huyo kuikabidhi Wizara hiyo                msaada wa magari tisa ya kuzima moto na uokoaji. Tukio la                makabidhiano ya magari hayo lilifanyika nje ya Jengo la                Wizara, jijini Dar es Salaam leo. 
                Wakuu wa Idara ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya                Nchi, Maafisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na                wageni waalikwa, wakimsikiliza Mkuu wa Jeshi hilo, Thobias                Andengenye (hayupo pichani) wakati alipokuwa anatoa hotuba                yake kabla ya Serikali ya Japan kutoa msaada wa magari                tisa ya kuzima moto na uokoaji. Tukio hilo lilifanyika nje                ya Jengo la Wizara, jijini Dar es Salaam. Katika hotuba                yake, Andengenye aliishukuru Serikali ya Japan kwa msaada                mkubwa ambao wameutoa kwa Jeshi lake. 
                Sehemu ya magari tisa yaliyokabidhiwa na Balozi wa                Japan, Masaharu Yoshiba kwa niaba ya Serikali yake yakiwa                nje ya Jengo la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Magari                hayo yaliyotolewa kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji                yalipokelewa na Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango, wa                Wizara hiyo, Haji Janabi, jijini Dar es Salaam leo. Picha                zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.