Kaimu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Michael John akizungumza na wandishi wa habari (hawapo
pichani) juu ya Takwimu za ugonjwa wa Kipindupindu zinaonyesha kuwa
mikoa ambayo ilikwishakupata ugonjwa imeongezeka na kufikia 23 baada ya
Mkoa wa Mtwara kuripoti wagonjwa wawili kuanzia jana tarehe 13 Machi
mwaka huu, katika wilaya ya Masasi. Mikoa ya Njombe na Ruvuma ndio
pekee hapa nchini ambayo bado haijaripoti mgonjwa wa Kipindupindu,
jijini Dar es Salaam leo, kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Kinga, wa
Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto,Dk,Neema
Rusibamayila.
Mkurugenzi
wa Huduma za Kinga, wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto, Dk. Neema Rusibamayila akizungumza na wandishi wa haari
(hawapo picha) juu ya Wizara inatoa wito kwa wadau wote katika ngazi
zote kushirikiana kwa pamoja katika jitihada za kutokomeza ugonjwa wa
kipindupindu, leo jijini Dar es Salaam.kulia ni Kaimu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto, Michael
John.
Wandishi
wa habari wakimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo
ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto, Michael John, jijini Dar es Salaam
leo.
(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii)
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
INAKADIRIWA
kuwa Sh.bilioni Mbili zimetumika katika harakati za kupambana na
ugonjwa wa kipindupindu tangu uliporipotiwa kwa mkoa wa Dar es Salaam.
Akizungumza
na waandishi habari jijini Dar es Salaam,kwa Niaba ya Naibu Waziri
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Kaimu Katibu wa
Wizara hiyo, Michael John, amesema kuwa serikali imeweka nguvu zaidi
katika kukabiliana na ugonjwa huo.
Amesema
fedha hizo zimetumika katika kuunda tume mbalimbali katika kutoa elimu
juu ya ugonjwa,vifaa pamoja na vitanda katika hospitali ambazo zilipatwa
na wagonjwa wa jamii hiyo.
Kaimu
Katibu Mkuu amesema Mikoa ya Kanda Ziwa imekuwa na imani potofu juu ya
kuchemsha maji ya kunywa kwa kudai kuwa ugonjwa huo unatokana na hali ya
hewa pamoja na wavuvi wa kanda hiyo kuwa wakinywa maji yaliyochemshwa
wanazma katika mitumbwi yao au wasiweze kuvua samaki hizo.
Amesema ugonjwa wa wa kipindupindu hapa nchini umedumu kwa takribani miezi saba (7) sasa tangu uanze mwezi Agosti, 2015.
John
amesema hadi kufikia Machi 13 mwaka huu jumla ya watu 18,399
wameugua ugonjwa huo, kati yao watu 292 wamepoteza maisha.
Takwimu
za ugonjwa huu pia zinaonyesha kuwa mikoa ambayo
ilikwishakupata ugonjwa imeongezeka na kufikia 23 baada ya Mkoa wa
Mtwara kuripoti wagonjwa wawili kuanzia jana ya machi 13 katika
wilaya ya Masasi.
Mikoa ya Njombe na Ruvuma ndio pekee hapa nchini ambayo bado haijaripoti mgonjwa wa Kipindupindu.
Takwimu
za wiki iliyopita kuanzia tarehe 7 hadi 13 Machi
2016 zinaonyesha kuwa, kasi ya ugonjwa wa kipindupindu
imeongezeka ambapo idadi ya wagonjwa walioripotiwa wiki hiyo
ni 758
Ikilinganishwa
na 544 wa wiki iliyotangulia ya tarehe 28 Februari hadi 6 Machi ambapo
ni ongezeko la asilimia 40. Mkoa wa Iringa ambao haukuwa umeripoti
wagonjwa wiki iliyotangulia, wiki hii imeripoti
Ugonjwa
katika Halmashauri ile ile ya Iringa, ambayo bado imeendelea
kuripotiwa ugonjwa wa kipindupindu pia imeongezeka kutoka 10 hadi 12.
Mikoa hiyo inaongozwa na Morogoro (196), Dodoma, (142),
Mwanza(108), Mara(86), Manyara(77), Iringa(77). Mikoa mingine
ni pamoja na, Dar es salaam(42), Mbeya(16), Arusha
(10),Lindi (2), Mtwara (2) na Rukwa (2).