Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Hassan Suluhu
akizungumza wakati wa siku ya Utepe Mweupe ambapo na uzinduzi wa kampeni
ya kuzuia vifo vya mama na mtoto katika mkutano uliofanyika katika
viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
Pia
mama Samia amewasihi wanawake kujiunga na mfuko wa jamii wa bima ya
afya ili kusaidia vituo vya afya. Pia amewataka wananchi kuachana na
mila potofu hasa za ukeketaji kwani ni kumkosoa mwenyezi Mwenyezi
Mungu.
Mganga
Mkuu wa Serikali, Profesa Mohamed Bakari Kambi akizungumza wakati wa
kuadhimisha siku ya Upete Mweupo kwa niaba ya Waziri wa Afya maendeleo
ya jamii, Jinsia, wazeee na watoto, Ummy Mwalimu leo katika uzinduzi wa
kampeni ya kuzuia vifo vya mama na mtoto katika viwanja vya Karimjee
jijini Dar es Salaam leo.
Mwakilishi
wa UNICEF akizungumza wakati wa kuadhimisha siku ya Utepe mweupe
ambapo mama Samia amezindua wa kampeni ya kuzuia vifo vya mama na mtoto
amesema atashirikiana vyema katika kuzuia vifo vya watoto wakati wa
kuzaliwa.
Mwakilishi
wa mganga mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Benedict Msiba akizungumza wakati wa
uzinduzi wa kampeni ya kuzuia vifo vya mama na mtoto wakati wa
kujifungua, ikiwa amesema kuwa katika mkoa wa Rukwa umejitahidi
kupunguza vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua.
shuhuda, Efrazia Saidia ambaye amenusurika kifo cha chake na mwanae kutokana na kuumwa uchungu kwa muda mrefu.

Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Hassan Suluhu
akionyesha vitabu ambavyo vimezinduliwa leo ambayo ni mpango wa serikali
kuendelea kuchangia kupunguza vifo vya mama na mtoto.

Baadhi
ya wananchi waliojitokeza katika siku ya Utepe mweupe jijini Dar es
Salaam leo na uzinduzi wa mpango mkakati wa kuzuia vifo vya mama na
mtoto wakati wa kujifungua.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Hassan Suluhu akiwa
katika picha ya pamoja na kamati ya maandalizi wa siku ya Utepe Mweupe
leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.