Friday, April 22, 2016

NICO NJOHOLE NA RENATUS NJOHOLE KUONGOZA SIMBA UGHAIBUNI, MPAMBANO WA WATANI WA JADI DALLAS


NICO NJOHOLE NA RENATUS NJOHOLE KUONGOZA SIMBA UGHAIBUNI, MPAMBANO WA WATANI WA JADI DALLAS
Kikosi cha Yanga ughaibuni
Kikosi cha Simba ughaibuni

Wanandugu wawili Nicodemus Njohole na Renatus Njohole ambao kwenye nyakati tofauti waliwahi kuchezea timu ya Simba ya jijini Dar es Salaam, wamethibitisha kuichezea timu ya Simba ughaibuni kwenye mpambano wa watani wa jadi utakaofanyika siku ya Jumamosi April 30, 2016 jijini Dallas, Texas nchini Marekani.

Hii itakua ni mara ya tatu kwa mpambano huu wa Simba na Yanga kuchezwa nje ya DC. Kama ilivyozoeleka watani hawa wa jadi mara nyingi mechi zao hufanyikia Washington, DC, na mara zote Yanga inaibuka mshindi.
Majimbo mengi ambako mpambano huu ulishawahi fanyika ni Columbus, Ohio na Houston, Texas.
Vijimambo ingiongea na Renatus Njohole kutokea nchini Switzerland na kuthibitisha kuiongoza Simba yeye na kaka yake Nico Njohole kwenye mpambano utakaochezwa Dallas katika kiwanja cha Hufthines Recreation Center ambacho anuani yake ni 200 N Piano Road, Richardson, TX 75081. Nicodemus yeye anaishi London, Uingereza.
Mapambano huu utakua wa wazi kwa mashabiki na wachezaji kujumuika pamoja na kuandika historia ambako kwa mara ya kwanza utaandika historia mpya ya kuchezwa na wachezaji wawili waliowahi kuichezea Club ya Simba. Michezo mingine iyakayokuwepo ni mpirsa wa kikapu na mpira wa wavu ikienda sambamba na nyama choma.
Mechi hii inayosubiliwa kwa hamu ni sehemu ya burudani itakayokuwepo kwenye kongamano la DICOTA ambalo mwaka huu linafanyika Dallas, Texas kuanzia April 28, mpaka May 1, 2016. Mashabiki na wachezaji wa pande zote wameanza kutupiana vijembe huku mashabiki wa Simba wakifurahia ujio wa Renatus Njohole na kaka yake Nico kuja kutia nguvu timu hiyo ambayo mechi nyingi za Simba na Yanga ughaibuni huishia kupata kipigo kutoka kwa mahasimu wao.
Timu ya Simba ughaibuni ina historia nzuri inapocheza nje ya DC, mara zote imeibuka mshindi.
Huu utakua mpambano wa pili wa Simba na Yanga kugombea kombe la DICOTA mara ya kwanza timu hizi zilikutana kwenye kongamano la DICOTA lililofanyika Washington, DC mwaka 2011 na kongamano hilo Rais mstaafu Mhe. Jakaya Kikwete ndiye aliyekua mgeni rasmi kwenye kongamano hilo..