Sunday, March 06, 2016

Blackfox yapata mwekezaji Kampuni ya mitindo yapata mwekezaji



Blackfox yapata mwekezaji Kampuni ya mitindo yapata mwekezaji
Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Blackfox Models Aj Mynah akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya kumpata muwekezaji ambae atawezesha kufungua ofisi itakayokuwa na sehemu ya kupigia picha na kufungua ofisi kwenye nchi nyingine mwaka ujao,katika mkutano uliofanyika leo jijini Daer es Salaam kushoto ni mwekezaji huyo David Johansson.
Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Blackfox Models Aj Mynah na mwekezaji huyo David Johansson wakisani mkataba katika mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Blackfox Models Aj Mynah akimkabidhi tishet mwekezaji huyo David Johansson leo jijini Daer es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Blackfox Models Aj Mynah na mwekezaji huyo David Johansson wakiwa katika picha ya pamoja na Models leo jijini Daer es Salaam.
KAMPUNI ya inayojishugulisha na masuala ya mitindo nchini Blackfox Modeling Agency imeahidi kuwaendeleza vijana zaidi katika fani hiyo baada ya kupata mwekezaji mpya kutokea nchini Uingereza.

Akizungumza na waandishi wa habari leo wakati wa utiaji wa saini wa mkataba wa makubaliano na mwekezaji huyo, mmiliki wa Blackfox Aj Mynah alisema kuwa hatua hiyo itafungua milango ya wanamitindo wa Tanzania nje ya nchi.Alisema kuwa mkataba huo unalenga kuiongezea nguvu zaidi kampuni ya BlackFox katika harakati zake za kuiendeleza fani ya mitindo nchini na kuifanya kuwa ya kimataifa zaidi.

"Kama inavyofahamika kuwa fani hii ya mitindo nchini sio kongwe sana ikilinganishwa na nchi nyingine hivyo basi makubaliano haya yanalenga kuifikisha kampuni ya Blackfox kuwa ya kimataifa zaidi inayoweza kusaidia mamilioni ya vijana sio tu hapa nchini bali hata nje ya Tanzania" alisema Aj.

Aliongeza kuwa kampuni hiyo inalenga kufungua milango nchi nyingine za Afrika Mashariki, Afrika na hata kwenda katika nchi za Ulaya na Amerika.Alisema kuwa kampuni hiyo imewandaa vijana wengi kuingia katika fani ya mitindo na kujiajili kama wanamitindo, matangazo na mengineo mengi.Alisema kuwa chini ya mkataba huo wanamitindo wa hapa nchini wataweza kwenda kufanya kazi katika nchi za Ulaya na kwengineko.

Kwa upande wake mwekezaji huyo David Johansson alisema kuwa ameamua kuingia mkataba na Black fox kutokana na fursa zilizopo hapa nchini kupitia fani hiyo.Alisema kuwa Tanzania inao wadada na wakaka ambao wanaweza kutangaza matangazo mbalimbali ya kimataifa na hata kufanya kazi nyingine zinazoendana na fani hiyo.